MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no, 0755683295/WatSap, Instagram @mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHU YA KUMI NA NANE.
Tulipoishia Nikamwona Zabroni akiondoka kwa kutembea na suti yake ya gharama haswaa. Nilijiona mjinga nisiye na akili ninayezidiwa na watoto wa mjini. Wakati naendesha gari mara nilihisi kama kitu nyuma ya gari. Nikageuka na kuona kuna______Enda nayo.....Kama kuna vifurushi viwili hivi. Sikua na kumbukumbu ya kuweka vifurushi kwenye gari langu yaani kwenye zile siti za nyuma. Nilitaka nisimame niangalie ni nini lakini foleni ilikua inasogea hivyo ikabidi niendeshe gari. Niliendesha huku nikitafuta sehemu ya kuchepuka ili nipaki gari niangalie vile vifurushi ni vya nini! Sikupata nafasi mpaka hapo niliposimamishwa na polisi wa usalama barabarani yaani traffic wakinihitaji kwa pembeni. Baada ya kusimama wakaniuliza leseni nikawapa. Kisha wakaniuliza kazi yangu nikawatolea kitambulisho cha kazi.
Baada ya kukiangalia wakasema samahani tunaomba kukagua gari yako. Kwa kua walikua kazini ikabidi niwaruhusu wakague tuu. Walianza kwenye buti, wakasema kuko sawa. Kisha wakaja kwenye siti za nyuma na kuniuliza vile vifurushi ni vya nini? Nikawajibu naombeni muangalie wenyewe. Kwani hata sijui vimefikaje humo. Basi traffic mmoja akaanza na mfuko wa kwanza kisha akaonekana kama aliyeshtuka sana. Nikamwuliza vipi? Akasema Afande ni nini hiki? haya si madawa ya kulevya? Nikauliza nini? Alipokua akifunua furushi la pili mshituko uliongezeka. Mungu wangu Maiti! Alitamka yule traffic. Nikasema mbona siwaelewi. Mmoja akajibu hii si gari yako? na umetuambia wewe ni askari kwa mjibu wa kitambulisho. Sasa je maiti na madawa unapeleka wapi?
Nilikua kama niliyemwagiwa maji ya baridi kwenye msimu wa baridi. Nilishindwa hata nijibu nini. Nilivuta kumbukumbu kama wakati napanda vitu vile vilikuwepo. Lakini sikupata jibu. Nikajua tuu wakati Zabroni amenizubaisha pale kwenye foleni ni hapo ndipo kuna wajinga wenzie wakaingiza madudu yao kwenye gari yangu. Nilibaki nimesimama mpaka hapo niliposikia Upo chini ya ulinzi mheshimiwa. Nilitakiwa kwenda kituoni mara moja. Nilitii amri kwani ni kweli mimi nilikutwa na hivyo vitu. Sikua na ujanja.
Moyo uliniuma afisa mzima nakamatwa na madawa ya kulevya. Zaidi maiti ya mtu. Haaa ilikua kituko haswaa. Basi nikapakizwa kwenye gari la polisi halafu yule afande mmoja akawa anaendesha gari langu. Tulifika kituoni na chaajabu ni kua nilikuta kikundi cha watu wakilia na kuonekana walikua wakinisubiri kwa shauku kubwa. Waliponiona waliinuka kwa hasira na kunivamia kwa ngumi na mateke huku wakidai nimemuua ndugu yao. Polisi wakajitahidi kuwazuia pale na mara baada ya kufanikiwa nikaingizwa kituoni. Huko nikakalishwa mkuu mmoja akaanza kwa kusema Afande yuu nakufahamu sana kwa uwajibikaji wako. Siamini haya ninayoyaona. Kisha akatoa kitu kama Cd (santuri) Akaiweka kwenye kompyuta na kunigeuzia.
Ndipo nilipojiona nafyatua risasi ovyo kwenye ile benki nilikokua nimetoka. Nilishtuka zaidi pale nilipomwona mtu akiuawa na kuburuzwa kutolewa kwa chini. Kumbe wale majambazi walichimba chini kwa chi na kutokezea kwenye benki kwa ndani. Hivyo ndo mana kikosi changu hakikuwaona. Kisha nikaonyeshwa kua yule aliyevutwa kuelekea shimoni alikua ni meneja wa benki. Aliuawa kikatili sana na ndiye aliyekutwa kwenye gari yangu. Hivyo ikaoneka mimi ndiye nilimwua na kutoka naye. Kisha nikamsikia yule afande akisema hao uliowaona hapo nje ni ndugu zake. Wana hasira na wewe sana wanajua umemuua ndugu yao.
Ilikua ni habari ya kushtusha sana kwangu. Yule aliyekua akionekana pale alikua ni Zabroni ambaye nimefanana naye kwa kila kitu. Kilichofanyika ni vibaraka wa Zabroni kuchukua tape za matukio zilizorekodiwa mle benki na CCTv kamera. Kisha wakaziwahisha polisi. Na wakati wamenizubaisha pale kwenye foleni ndipo waliingiza madawa na maiti ya yule meneja wa benki. Hivyo kwa haraka kila mtu akajua mimi ndiye niliyehusika. Haah! Kucheza na Zabroni makweka ilikua inahitaji nguvu ya ziada. Alikua mwingi wa ubunifu na udanganyifu. Alikua ana uwezo wa kulitengeneza tukio na kulifanya lionekane kweli. Hakika niliishiwa pozi. Nilibaki nimekaa nisijue chakujibu. Hakika waliniweza.
Baada ya mahojiano ya mda mrefu na kuwaeleza jinsi tukio lilivyo. Wao wakadai kua wamenielewa lakini ndugu wa marehemu hawatanielewa kwasababu na wao walipewa kopi ya ile Cd, Na aliyewapa inasemekana ni kibaraka wa Zabroni. Hakika walifanikiwa kunichafua haswaa. Hivyo hapakua na jinsi zaidi ya kuwasikiliza wao wanasema nini. Akatoka askari mmoja na kuwaomba watulie nao wakatii. Kisha akajaribu kuwaelewesha kua mimi si yule aliyeonekana kwenye CD, Kwa mara nyingine makovu yakasaidia kunitofautisha na Zabroni. Walionekana kuelewa. Wakaomba ruhusa ya kuchukua mwili wa ndugu yao. Wakachukua na kuondoka zao bila kuongea lolote.
Baada ya askari yule kurudi akasema sasa Afande yuu pole sana. Nikajibu ahsante. Kisha akasema bwana tukuombe urudi hapa kesho ili tumalize hili swala mana tunajua leo ulikua unashuhulikia swala hilo la uvamizi wa benki. Niliwashukuru sana kwa ushirikiano wao. Hakika kwenye ukweli uwongo hujitenga. Mimi sikudhani kama ningetoka nilijua ni jela tuu hakuna kingine. Niliwashukuru sana kisha nikawaomba gale madawa wateketeze kwa moto. Mimi nikaondoka huku kichwani nikiwa na mawazo sana.
Niliendesha gari huku kichwa changu kikiwa kimejaa mawazo. Nilikua namuwaza huyu Zabroni ni mtu wa namna gani. Mbona ana michezo ya hatari. Nikiwa bara barani kwa mbali nikamwona mtu kama Peris akiwa ameshikana mkono na mtu ambaye nilidhani ni Zabroni. Walikua wakielekea mlango fulani wa gesti. Nikapatwa na hasira sana nikapaki gari haraka na kushuka kuwakimbilia huku nikijiapiza kuua. Niliwakimbilia mpaka nikawakuta. Niliita jina Perisi. Hawakugeuka nikaamua liwalo na lowe nikaamua kumpapasa begani Peris mara wote wakageuka Mshituko mkubwa ukanipata kwani______ ______________________________
EmoticonEmoticon