MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no, 0755683295/Watsap,Email@
Tulipoishia Mpaka naondoka katika lile jumba. Mwisho wa ile video yakatokea maandishi "BROUGHT TO YOU BY ZABRONI MAKWEKA COMPANY" Nikameza mate funda moja.mara nikasikia mlango unagongwa ngo! Ngo! Ngo!____Enda nayo..........Niliingiwa na woga kiasi. Nikajiuliza ni nani anaweza kuwa anagong mda ule lakini majibu sikupata. Nikanuka haraka na kuficha vile vitu nilivyokusanya kisha nikaenda kufungua mlango. Wakati nafungua mlango nikakutana na Peris katoka kazini. Akaniuliza vipi tena mume wangu mbona unajifungia? Nikamjibu aah sasahivi naishi kwa mashaka sana hivyo kujilinda muhimu sana. Pole mume wangu yatakwisha tuu. Nikamjibu na yatakwisha ndiyo maana tunakoelekea ni mwisho wa mlolongo mrefu. Alionekana kutahamaki kiasi kisha akasema kwani vipi ushawajua wabaya wako? Nikajibu hapana namwachia Mungu amalizane nao na kwakua Mungu mi mwaminifu basi atatenda juu ya hili.
Nilimjibu vile kwa makusudi kabisa ili ajue kua tayari na yeye nimemjua ya kua si mtu mzuri. Basi tukaingia ndani mimi nikarudi kukaa pale kwenye Laptop yangu na kuangalia vitu kadhaa kisha nikaizima. Mda ikasonga usiku ukapita asubuhi kukakucha shuhuli zikachukua mkondo wake.Nikiwa natafakari jinsi ya kuendelea na ile kesi sikua najali vitisho vya Zabroni tena. Nilijitoa muhanga na kusema sina kinachonililia zaidi ya nchi yangu ya Tanzania. Nikaamua niende sehemu moja hivi huko miliwahi pata taarifa kua Zabroni ni maeneo yake ya starehe. Nikawasha gari na taratibu kabsa nikaanza kusogea maeneo hayo. Lakini nikiwa njiani naenda kuna kitu cha tofauti nilikihisi. Niliona kuna pikipiki kama sita hivi nyuma yangu. Baada ya kuzitilia mashaka nikaona dawa ni moja tuu. Nikaongeza mwendo nao wakaongeza nikajua natimiza lengo. Nikasimamisha gari kwa ghafla wakajigonga na kupata ajali mbaya pale.
Sikutaka kupoteza mda wa kuwaangali kwani ningekutwa na polisi. Nikawasha gari na kutokomea zangu. Nilifika lile eneo na nilikaa kwa mda mrefu lakini sikubahatika kumwona Zabroni. Nikakata tamaa na kuamua kurudisha silaha zangu yaani kisu na bastola kwenye gari. Nikarudi kukaa nikiwa mtupu kabsa sina silaha yoyote. Kwakua ile ilikua ni hotel nikawa naendelea kupata huduma huku nikifikiria jinsi ya kumkabili Zabroni. Nikasikia ujumbe mfupi umeingia kwenye simu yangu nao ulisomeka hivi "KAKA VIPI NIMEKUONA MDA MREFU HAPO" Wakati nataka kuangalia namba iliyotuma mara nikasikia mtu akiwa amesimama mbele yangu akisema. Unanitafuta mimi ee? Nimekuona mda mrefu hapa.
Nilipoinua kichwa na kutazama ni nani roho ililipuka kwa gadhabu. Alikua ni Zabroni mbele ya macho yangu. Alikua kanitegea bastola chini ya meza hivyo ningepigwa maeneo ya tumbo. Haikua raisi kwa wengine kumwona kutokana meza yangu kumzuia. Basi nikabaki nimeachia mdomo nisijue la kufanya. Nijamsikia akisema najua unanitafuta mimi sasa sikia. Hua sikamatwi kirahisi kama unavyoniwazia. Nilikuona tangu unafika na nimeamua kukusaidia kukulipia bili yako ili usike ukatumia pesa yingi kwaajili yangu. Nilihesabu vitu ulivyotumia na nilipojua nikaende kaunta kulipia. Nimelipa na kuacha chenji hivyo endelea kutumia chenji iliyobaki. Pole sana afande Yuu hii michezo ya wakubwa.
Sikuongea neno lolote Zabroni akaanza kuondoka zake. Ilikua ni dharau ya hali ya juu. Nilijiona bwege nisiye tumia akili kabisaa. Nikatamani nimfuate lakini tayari yeye alikua na silaha hivyo ilikua ni rahisi mimi kuuawa. Nilipoinuka kwenda kulipa bili yangu nikaambiwa tayari imelipwa. Mmmh hakika Zabroni alikua ni mjanja na mwelevu sana. Nikaamua kuondoka kwa hasira na kurudi nyumbani. Nilipofika nyumbani nilipigiwa simu na afande mwenzangu wa kituo kimoja nikamsikia akisema Yuu nimevamiwa msaaaa......... Mara simu ikakatika. Nilijua itakua nyumbani kwake tuu.
Nilitoka mbio kuwahi ili hata nijaribu kuokoa maisha yake. Haikua mbali mara nikafika mle ndani na kukuta kukiwa kumetulia. Niliingia na kuwakuta watu watatu wamelala na nilipowachunguza nikagundua wamepigwa risasi. Nikaamua kutoa silaha yangu ili kama kuna hatari nikabiliane nayo. Mara nikiwa nimeshikilia bastola nilishtuka kama kuna mwanga wa kamera unaonimulika mara kwa mara. Ilikua ni kiashiria tosha ya kua napigwa picha. Nikaangalia huku na huko mpiga picha simwoni na kwa vyovyote kwa zile picha na jinsi mauaji yalivyotokea kwa kupigwa risasi na mimi ndiye nimeshika bastola lazima ningeonekana mimi ndiye nimeua.
Hivyo ilinilazimu kuacha kuangalia usalama wa mle ndani. Nimtafute kwanza mpiga picha anayepiga picha kwa mfululizo. Nikapepesa macho huku na huko simwoni mara nikamwona kwenyedirisha moja wapo. Nikaamua kutoka na kumkamata. Wakati natoka huku mbele yeye naye akatokomea kusikojulikana hivyo sikubahatika kumwona hata sura. Alikua wa kike au wa kiume sikujua. Nilijaribu kuzunguka lile eneo lote sikuona kitu. Nikaona njia pekee ya kuokoka ni kutoweka eneo lile mara moja.Ikumbukwe pia nilikatazwa kujihusisha na shughuli zozote za kiusalama. Na endapo ningefanya hivyo ningechukuliwa kama mhalifu wa nchi.
Nilifika nyumbani kwangu na kuanza kuumiza kichwa. Nilikua natafakari ni nani kanipiga picha na kwa malengo gani? Kile kitu kilikua kinanitesa sana. Afadhali hata ningemwona mtu mwenyewe japo kwa sura. Lakini sikumwona hivyo kumtambua haitawezekana. Nikajikaumu kwa kwenda kwa haraka kumsaidia askari mwenzangu aliyekua kavamiwa. Kila nilichokua nafanya ilikua ni kukosea tuu kiukweli Zabroni alinimaliza kiakili. Aliua watu wengi na bado na mimi nilikuwemo kwenye orodha. ;Kilichokua kinanisaidia mimi ni kwamba nilitakiwa kuuawa mwishoni baada ya wao kuua wote. Sikutaka kukubaliana na hilo. Japo tayari Zabroni alikua ameniweza kwa kunichezea mara nyingi.
Nilikaa pale kwenye kochi nikitafakari ni nini nifanye lakini majibu nilikosa. Hivi ni kweli nimeshindwa kumkamata Zabroni? Hivi ni kweli afisa mzima mzima napigwa picha halafu nakua mwoga? Nini maana ya kusoma sasa. Nakaa nyumbani kwangu najifungia kweli? Naishi kwa mashaka je raia wa kawaida waishije sasa? Nikiwa najiuliza hayo maswali mara nikaona damu inatiririka chini ya mlango wangu ikitokea nje kuingia ndani.-_______________________
EmoticonEmoticon