SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?SEHEMU YA 29

 Displaying sehemu ya 29.jpg

MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com, instagram@mwalim_yuu.Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala..

SEHEMU YA 29.
Tulipoishia, Nilipofika na kushika kichwa kiliporomoka na kuanguka chini. Alikua kashakatwa kichwa kwamana ni mfu tayari. Nikiwa nawaza nini nifanye mara ghafla_____Enda nayo....... Nikasikia mlango unagongwa. Nikiwa nimeduwaa najiuliza nifanye waliingia askari wakiwa wameshikilia mitutu ya bunduki kisha wakasema hapohapo ulipi inua mikono juu. Uko chini ya ulinzi. Niliinua mkkono afande mmoja akaja na kunifunga pingu kisha wakaniamuru kutoka nje na kwenda kituoni. Nilitii baada ya kufika kituoni niliingizwa mahabusu na kulala humo usiku ule. Asubuhi nilifuatwa na kuambiwa kesi yangu tayari iko mahakamani na nahitajika kwenda kujibu mashitaka. Nilitolewa nikapandishwa kwenye karandinga kuelekea mahakamani.

Tulifika mahakama ya Kisutu kesi yangu ikawa kesi ya kwanza kusomwa. Nilisomewa mashitaka mawili ambapo moja ilikua ni kuua bila kukusudia, na la pili ni udanganyifu ambapo nilimdanganya mkuu wa kituo kua aje nyumbani kwangu ili tumalize ugomvi wetu na alipofika nikamuua kwa kumchoma visu. Vielelezo vya ushahidi vikaletwa kwanza ni mawasiliano ya simu ambapo ilionekana namba yangu ilikua ikiwasiliana na Marehemu huku nikimshawishi aje nyumbani kwangu tuyamalize. Ushahidi wa pili ni mkanda wa video ambao ulirekodiwa kwa siri mimi nikiwa namuua Mkuu wangu pale nyumbani kwangu. Chaajabu ni kua ni kweli muuaji aliyekua akionekana alikua ni mimi.

Ushahidi wa tatu alikua ni shuhuda aliyenishuhudia kwa macho yake. Kwaamara ya kwanza nikamwona Peris akisimama na kuthibitisha kua mimi ndiye niliyeua na yeye ndiye alinirekodi. Hapakua na mda wa kuuliza Peris alikua wapi na kwanini aliacha kazi ghafla. Hayo yote yalifunikwa mimi tuu ndo nilikua naangaliwa. Maswali kichwqni yalijaa nikiwa najiuliza ni kesi gani hapa Tanzania ilifanyiwa uchunguzi ndani ya usiku mmoja na ushahidi kukamilika? Mbona kesi yangu ilichukua mda mfupi sana. Kuna watu miaka saba hua mahabusu kesi yangu imewezekanaje? Na pili kwanini nihukumiwe kwa kosa la kuua bila kukusudia ikiwa mimi ndiye nilimwita na kumuua. Zaidi nikajiuliza Peris alipiga picha na kuzipeleka polisi je mbona hawakumkamata wakati ni mtuhumiwa.

Maswali yalikua mengi ambayo hata majibu nilikuwa sina. Nilipigwa na butwa uchungu ukanitawala. Nikamlaani Zabroni, nikamlaani Peris, Nikalaani jeshi la polisi kwa kushindwa japo kunitetea hata kidogo. Zaidi wao waliongeza ushahidi wa kuwa nilikuwa na ugomvi na marehemu hivyo nimemuua kwa makusudi. Nililaumu sana machozi yalinitoka bila kikomo afande nilimwaga chozi kizimbani. Kisha nikamsikia hakimu mfawidhi wa mahakana ya Kisutu akiuliza je mshitakiwa una utetezi wowote juu ya haya yote?

Sikua na la kuongea zaidi ya kulia tuu kwa uchungu. Aliuliza tena una utetezi? Nikajibu kwa gadhabu sina utetezi zaidi ya kusema mimi sihusiki. Basi hakimu akasoma hukumu na kusema Ndugu Yusuph Abel Ng'ahala unahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na hukumu hiyo utaanza kuitumikia sasa hivi. Nilishangaa kesi gani ya mauaji ufungwe miaka mitano? Nilijiuliza mambo mengi nadhani kesi yangu iliweka rekodi ya kua kesi pekee iliyochukua mda mfupi kuichunguza na kuitolea hukumu. Hakuna kesi hapa Tanzania iliyowahi kusomwa na kwa mda mfupi kama yangu nadhani kuna namna iliamrishwa nifungwe ili watu wengine waendelee na mambo yao kwa uhuru.

Nililia sana kama mtoto mdogo. Askari walikuja wakanitoa kizimbaniyangu.unipeleka kwenye karandinga. Nikakaa kusubiri wenzangu. Afisa upelelezi nilifungwa pingu kwa kosa ambalo sikulifanya, afisa mzima niliwekwa chini ya ulinzi sasa. Afisa mzima wa upelelezi nikahukumiwa kwa kosa la uuaji. Haki iko wapi Tanzania, haki iko wapi, nani anasimamia haki ikiwa hata mahakama haikuchunguza kwa makini. Je wanyonge twende wapi jamani Nalia na tanzania naipenda Tanzania niliapa kuipigania mpaka nakufa lakini mbona nalipwa nisichostahili. Serikali yangu iko wapi, Sheeia mbona wanazijua wachache nililia sana huku nikitafakari mambo mengi sana.

Nilipambana kila nilipopaswa kulitetea taifa la Tanzania, niliapa kuilinda mpaka kufa nilitamani amani na upendo aliouacha mwalimu Julius kambarage Nyerere udumu miongoni mwetu. Sikupenda watu wachache kama Zabroni waharibu amani yetu. Nilitamani siku moja nione kila mtu anafurahia mema ya Tanzania naipenda nchi yangu. Nilijikuta naimba wimbo wa zamani kidogo huku nalia. Nilitiririka machozi ndani ya karandinga huku nikiimba.

"Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wotee!
Nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana!
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee!
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo woteeeee!!!"

Wakati namaliza kuimba niliwafanya wale maaskari magereza kubaki wameduwaa wakiniangalia na kunishangaa. Niliipenda nchi yangu lakini ni watu wachache wakafanya niwe kama msaliti kwa taifa langu. Kwanini lakini sikuangaliwa mema yangu niliyofanya nikiwa na jeshi la polisi. Kwanini sikuchunguzwa kama wengine. Kwanini sheria haikuangaliwa mara mbili hatimae ikamuhukumu mtu asiye na hatia. Tunaipeleka wapi nchi kwa mwenendo kama huu?

Sikua na jinsi wala lingine la kufanya. Nilimkumbuka mama kijijini ananitegemea. Baba alitegemea uwepo wangu Kaka zangu walikuwa hawana mbele wala nyuma mimi ndo kilikuwa kichwa cha familia na sasa naenda jela. Baba na mama wataishi vipi. Maisha yalibadilika ghafla kutoka kwenye uzuri na kuwa mabaya yasiyofaa hata kidogo. Nilihisi dunia imenitenga. Nililia sana kwakweli sikuona mchango wangu kuthaminiwa na taifa hili. Nikiwa bado nalia kwa uchungu mara kuna wengine watatu wakaongezeka mle kwenye karandinga kisha gari taratibu ikaanza safari kuelekea jela. Huko ndiko tulipaswa kutumikia vifungo vyetu hakika inauma________________________
_______________________________________________________________________________________________________________________________Simulizi ndo kwanza inaanza, kutana na mimi sehemu ya 30 tujue yaliyojiri huko jela. Kwa lolote nicheki kwa mawasiliano hayo hapo juu. Hebu wote tumalize kwa kusema Amani na Upendo daima Tunaipenda Afrika yetu, Nakupenda Tanzania. Bye bye bye
Previous
Next Post »