MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com, Instagram@mwalim_yuu, Fb.co/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 28.
Tulipoishia, Akaanguka nikamsachi kama anachochote ndipo niligundua alikua na silaha moja tuu bastola ndogo. Pia nikagundua alikua ni mwanamke. Wakati nainuka nisonge mbele nikasikia___Songa nayo....... Sauti ikiongea kwa kunong'ona ikisema Brother pita kule mi napita huku tuwaweke katikati ili tuwaue wote. Nilishtuka kiasi nikamwangalia kisha nikasikia tena brothe mi ni Oscar nilikufuata nyumanyuma. Aaah kwakua haikua mahali pazuri kubishania nikamwambia poa pita korido hiyo. Akasonga na mimi nikasonga mbele.
Nikasogea nikakuta kikundi cha vijana watatu wakiwa wanavuta sigara. Walikua kwenye chumba fulani. Nikakaa kuangalia naanzaje. Walikua bado hawajashtuka kama kuna mtu kaingia. Nikiwa natafakari kumbe Oscar alikua tayari kaingia ila kabana ukutani. Nilipomwona nikaona kazi imekua nyepesi nilivamia pale kwa ghafla nikamchoma mmoja kisu cha kichwani eneo la utosi. Mara Oscar naye akazidisha shambulizi kwa risasi wale wawili waliobaki. Hapo kazi ikawa imekamilika kimya kimya. Tulitoka na kutafuta vyumba vingine lakini hatukuona kitu.
Nilijua kwa siku ile wale ndio walikuwamo. Nikamwambia Oscar tutoweke haraka. Tulipotea salama na kurudi nyumbani sikumlaumu sana Oscar kwani alinisaidia sana. Basi usiku ule nikalala kama sijui kilichojiri asubuhi nikawahi kazini. Kisha nikawahi sehemu moja hivi kuna taarifa za kiintelijensia nilipata kua kuna hisia kuna magari yanapita si salama. Niliwashitukiza askari bila kuwambia tunaenda wapi? Baada ya kufika eneo lile tukawa tunakagua kila gari. Mara kuna magari yalikua matatu yalikua yamewasha taa kuashiria wamebeba maiti. Kisheria tulipswa kuwaruhusu lakini akili yangu iligoma.
Nikawaamuru wapaki kisha nikaanza ukaguzi. Maiti ya kwanza niliiangalia ilikua imeuawa. Nikawauliza kama wana kibali chochote cha polisi wakasema hapana. Na nilipoiangalia sana ule uuaji ni wangu. Nikajua ni zile maiti za jana. Nikaamuru askari mmoja aniletee kifaa fulani cha kukagulia madawa ya kulevya. Na alipofika tuu kile kifaa kikaanza kupiga kelele. Hapo nikajua zile maiti si salama nikaifungua moja ma kukuta imeshonwa na nyuzi tumboni kama gunia.
Ilikua ni uchungu kuliko kawaida. Baada ya kuangalia kumbe ndani mlikua na madawa aina ya "cocaine" wakati nazidi kukagua gari ya pili hapo ndipo moto ukawaka. Walitokea watu na gari ndogo nyeusi wakaaanza kumimina risasi upande wetu. Hali ile ilinifanya nitafute mahali nianze kujibu mashambulizi. Askari wengine nao walianza kujibu lakini kwakua tulikua wachache na hatukujua askari wanne waliuawa paleale tukabaki wawili.
Wakati tunang'ang'ana kupambana nao zile gari zenye maiti zikaanza kuondoka kwa kasi kisha zikapotea. Hatukua na ujanja zaidi tulibaki wawili hivyo tulilazimika kuponya roho zetu. Kisha na kile kigari kidogo kikatoweka huku wakiwa wamepiga bomu la machozi na kutufanya tusione wanakoelekea. Baada ya dakika kadhaa wananchi walijaa eneo lile wakitupa pole. Nililaumu sana kitendo cha kutembea na askari wachache. Majambazi hawana huruma yani kitendo cha mimi kuua vijakazi wao kwao haikua na hasara hata kidogo. Kwao ilikua faida kwani walipata maiti za kusafirishia madawa Eee Mungu tuhurumie sisi wanadamu wenye laana.
Wakati nataka nipige simu kituo cha mbele kwamba zile gari wazizuie. Simu ilikua haiwaki. Sikujua tatizo ni nini. Nikapakia wale askari wenzangu kwenye difenda ili turudi kituoni. Baada ya kufika kiuoni wenzetu walitjpokea kwa huzuni lakini wangefanya nini unadhani? Kulikua hakuna ujanja tena. Nilikua nimechoka haswaa akili yanguilikua imefika ukomo wa kufikiria. Mara tukiwa pale mkuu akaja na kuanza kugomba sana mbele ya maaskari wenzetu. Alidai ni uzembe.
Kitendo kile kiliniudhi sana. Hakujua hata kwa njia gani tumepambana halafu anakuja na kusema ni uzembe nilichukia sana. Nilianza kumjibu kwa jaziba. Kuna maafisa wenzangu wakawa wananituliza. Alizidi kupayuka vitu vya kijinga akilaumu vitu ambavyo havijui nikaona hata kama ni mkuu wangu wa kazi wacha nimfundishe adabu. Niliwasukuma kwa nguvu wale walionishika kisha nikamfuata nikamtia makofi mawili ya akili halafu nikamwangalia kwa hasira.
Aliniangalia huku mdomo ukiwa unavuja damu na jicho lisiloamini kilichotokea. Nikamwambia mkuu kama ni upolisi bora kulima, Nimepigania vyakutosha, Nimepambana vyakutosha, Nimesingiziwa mangapi, Nimelitetea taifa hili mangapi? Nimempoteza mke wangu, kisa kazi, nimempoteza mwanangu kifo cha aibu kisa kutetea Nchi yangu, niliachishwa kazi, mkanirudisha wakati wa shida sikukataa nikarudi. Na leo nimepambana hadi kuhatarisha maisha yangu halafu unaongea upuuzi hapa eti uzembe. Kama ni uzembe nivye kila kinachohusika n jeshi hapa nibaki raia wa kawaida. Vua vuaaaaa!
Niliongea kwa uchungu sana. Kimya kilitawala kwa kila aliyekuwepo pale. Wote waliogopa hata kunisogelea nilikua nimegadhabika kwa kuona pamoja na kujituma kote lakini juhudi zangu ni buree. Hali ile ilimfanya mkuu kuondoka nadhani aligundua kua kanikosea. Baada ya kuondoka na mimi nikarudi ofisini kwangu nikawa napanga jinsi ya kulianzia usiku ule moto ni uleule. Mda ukasonga na kusogea kisha jioni ikafika. Nilitoka na kupitia ofisini kwa mkuu nikamwombe radhi japo yeye ndiye alianza kunikosea. Nilipofika ofisini kwake sikumkuta nadhani alikua ameshaondoka.
Na mimi nikawasha pikipiki yangu na kuondoka. Nilifika nyumbani na kupaki pikipiki yangu. Taratibu nikawa najongea ndani mwangu. Nilifika mlangoni na kuusukuma ukafunguka haukua umefungwa. Ile naingia macho yangu yakatua moja kwa moja kwenye kochi ambalo alionekana mtu kakaa pale. Niliposogea niligundua ni mkuu wangu wa kazi akiwa kachomwa visu shingoni na tumboni tena havijachomolewa vipo. Woga ukanijaa nikaanza kumsogelea ili nijue kama kafa au mzima. Nilipofika na kushika kichwa kiliporomoka na kuanguka chini. Alikua kashakatwa kichwa kwamana ni mfu tayari. Nikiwa nawaza nini nifanye mara ghafla________________________
EmoticonEmoticon