MTU MMOJA AMEKUTWA AKIWA AMEKUFA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI HUKU MWILI WAKE UKIKUTWA NA DAWA ZINAZODHANIWA KUWA NI ZA KULEVYA



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 18.05.2015.

·        MTU MMOJA KATI YA WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI.


·        MTU MMOJA AMEKUTWA AKIWA AMEKUFA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI HUKU MWILI WAKE UKIKUTWA NA DAWA ZINAZODHANIWA KUWA NI ZA KULEVYA.


·        MKAZI MMOJA WA KIJIJI CHA SHIGAMBA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI ACHOMEWA NYUMBA MOTO NA KUTEKETEZA VITU VYENYE THAMANI YA TSHS. 8,000,000/=.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA KATI YA WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI NA KISHA KUCHOMWA MOTO MARA BAADA YA KUMVAMIA JULIUS MKEA (60) MKAZI WA IFUMBO NA KUMPORA PESA TSHS 3,000,000/= WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA S/GUN YENYE NAMBA R 58308 LSA 1961.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 17.05.2015 MAJIRA YA SAA 21:30 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA IFUMBO, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.


AIDHA KATIKA TUKIO HILO, PIKIPIKI MBILI ZENYE NAMBA ZA USAJILI T. 507 DAN NA T. 924 CAM ZOTE AINA YA T-BETTER ZILIKUWA ZIKITUMIWA NA WATUHUMIWA ZILIKAMATWA. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WAWILI WALIOKIMBIA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI NA KUKIMBIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


KATIKA TUKIO LA PILI:

 MNAMO TAREHE 17/5/2015 JIONI  MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ATHUMAN OMARY ABDALLAH (37) MTANZANIA MWENYE PASSPORT NO. AB 452347 ILIYOTOLEWA DSM TAREHE 11.02.2011. ALIKUTWA AMEKUFA CHUMBANI HUKO KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO MIAMI GUEST CHUMBA NAMBA 208.

MWILI WA MAREHEMU HUYO UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI YA VWAWA WILAYA YA MBOZI KUSUBIRI KUTAMBULIWA. AIDHA MAREHEMU ALIFIKA KATIKA NYUMBA HIYO TAREHE 15.05.2015 JIONI KWA USAFIRI WA BASI LA FALCON AKITOKEA DAR ES SALAAM.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KAMA KUNA MTU KAPOTELEWA NA NDUGU YAKE AFIKE HOSPITALINI HAPO ILI KUTAMBUA MWILI HUO.

 
KATIKA TUKIO LA TATU:

MKAZI MMOJA WA KIJIJI CHA SHIGAMBA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA RED KAMETA (47) MFANYABIASHARA ALICHOMEWA MOTO NYUMBA YAKE NA KUTEKETEZWA VITU VYENYE THAMANI YA TSHS 8,000,000/=.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 17.05.2015 MAJIRA YA SAA 20:45 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHIGAMBA, KATA YA IWINDI, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.

MTILIWA SHAKA NI MKWE WA MHANGA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA CHRISTIAN. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. MOTO HUO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO WA WANANCHI WA KIJIJI HICHO. CHANZO CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. UPELELEZI UNAENDELEA.


Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng