MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA:
Sim no,0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com, Instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 27.
Tulipoishia, Mbona unatushangaza umerudu kuuliza tena. Nilijua tuu huenda Zabroni kapita. Nikiwa nimeduwaa mara simu yangu ikaita kuangalia nani anapiga alikua ni Peris nikapokea kisha nikasikia___Endelea...........
Niliamua kumwaga nesi pale na kumuomba samahani kwa usumbufu. Nikarudi ofisini na kukaa kutafakari njia gani nitumie. Nikaamua moja tuu niwafuatilie kwa siri mimi peke yangu na kila nikimkamata mmoja naua. Baada ya kuona ni wazo jema nikamfuata mkuu wa kituo kumshirikisha. Nikamweleza naye akakubaliana na wazo langu lakini pia akasema mimi nifuatilie kimya kimya lakini yeye pia ataweka askari kadhaa washughulike na swala lile ila wao watakua kimpango wao. Mimi pia nikakubali hilo swala na kumuunga mkono.
Basi kwakua tayari niliamua kuanza kazi mda huo huo nilitoka na kuanza kazi yangu. Nilitembelea kampuni ya simu ya mtandao fulani kisha nikamfuata injinia wa mawasiliano. Nikampa namba zile za Peris na Zabroni ili anionyeshe kwa wakati ule zinaonyesha wako wapi? Kwakua nilimwonyesha kitambulisho alionyesha ushirikiano wa kutosha sana. Baada ya mda akasema namba ya Zabroni haionyeshi chochote. Akaongeza kua ile ni mbinu ambayo imekua ikitumiwa na majambazi wakubwa Nchi kama Marekani na Wingereza. Hufanya hivyo ili kukwepa kukamatwa hivyo njia pekee ni kusubiri akipiga ndipo tuichukue. Ila ya Peris ilionyesha yupo maeneo ya Ubungo kwenye jengo flani. Basi nilimshukuru na kumwachia namba yangu ya mawasiliano kama kutakua na chochote anitaarifu.
Nilitoka hadi ubungo ambapo nilionyeshwa kua nba ile na mmiliki yuko maeneo hayo. Nilishuka kwenye gari na kuanza kula mingo maeneo yale. Nilisogea kwa mbele kiasi lakininikawa sioni kitu. Nilizunguka sana lakini wapi. Hali ya kukata tamaa ikaniingia nikajisemea kama kashaondoka basi. Nikarudi kwenye gari na kuliwasha ili niondoke. Wakati nawasha mlango niliuacha wazi basi kuna kipofu akawa anapita na fimbo mpaka kwenye mlango. Nililazimika kushuka na kumsaidia kwakua nilijua sitamfikisha mbali nikaacha gari inawaka.
Ghafla kwa nyuma nikashanga gari inaondolewa na nilipogeuka hata yule kipofu sikumwona tena. Nilishtuka sana nilipigwa na butwaa hata kupiga kelele za mwizi nikashindwa. Nikabaki nimesimama pale mikono kichwani kama nisiyejua lakufanya. Mar kwa mbaali nikamwona Peris na Zabroni wakiingia jengo la Ubungo Plaza. Walikua wameshikana mikono. Nilijikuta nasahau kama nimeibiwa gari nikatoka mbio kuwafuatilia. Nilifika mlangoni wao wakawa wameshaingia. Nilipoingia mle ndani nikapepesa macho sikuwaona nilikua naona nyuso ngeni tuu.
Nilizunguka mle ndani lakini wapi! Nilijitahidi kukagua hapa na pale sikuona kitu. Nikamfuata jamaa mmoja alikua pale mlango nikamwuliza vipi kuna jamaa kaingia na mtu wameshikana hapa kaelekea wapi? Haaa we mwehu nini mi nitaangalia wangapi ebu nipishe huko ebo! Alimaliza yule kijana akinisukuma. Nilijisikia vibaya sana nikaamua kuondoka zangu huku nikiwa na uchungu wa kuibiwa gari langu. Wakati natoka niko nje nikapigiwa simu kuangalia alikua ni Peris nikachukia sana nikapokea nikasikia geuka nyuma. Ile nageuka nikawaona wakiwa kwenye moja kati ya madirisha ya Ubungo plaza wakinipungia mikono.
Niligadhabika na kuamua kurudi nakimbia. Nilipofika mlangoni mlinzi naye akanisimanisha. Aiser fipi mbona sikuerewi rafiki? Aliuliza yule mlinzi mwemye rafudhi ya kimasai. Nikamtolea kitambulisho kisha akanywea mi nikaangia haraka lakini nikawa tayari nimechelewa. Kwani kila nilipoangaza Pale sikuwaona. Nilijilaumu sana lakini ningefanya nini. Nikaamua kuondoka na kurudi kituoni nikajipange.
Wakati natoka nilienda moja kwa moja kwenye daladala na kupanda. Nikiwa njiani nikapokea ujumbe mfupi wa maneno uliosomeka Gari yako tunayo sisi poleee. Ulikua unasomeka kama ujumbe uliutumwa na kampuni ambapo nikitaka kupiga namba hakuna ila jina linaonyesha Zabroni. Aaah nilijikuta naguna kwa hasira. Nilifika kituoni nikawapa taarifa askari wenzangu ya kua gari yangu nimeibiwa hivyo wakiiona popote wamkamate mtumiaji na aletwe. Mda ukasonga kisha usiku ukaingia mimi nikarudi nyumbani ili nianze operation ya kukamata na kuua usiku ule. Tayari nilipata taarifa za siri na sikutaka kumwambia yeyote taarifa hizi zilikua zinaonyesha mahali walipo majambazi wale kwa usiku ule.
Nilibeba visu vyangu viwili vikali haswaa, na pia bastola mbili nikavaa kikazi zaidi na kuondoka. Oscar alitaka twende wote nikamkatalia na kumwambia abaki nyumbani. Nilifika kwenye ile nyumba niliyoelekezwa na kuanza na mlinzi. Sikua na huruma nilimkata kichwa na kumtupia huko. Nikasonga ndani kwa kunyata. Nikajibanza kwenye korido mara kuna mtu akawa anatoka nje anaingia ndani nikamsubiria kwa tahadhari kisha nikamziba mdomo na kumchoma kisu cha tumbo akaanguka nikamlaza kimya kimya halafu nikanyata kusogea mbele zaidi.
Nilisogea na kisha nikaamua nijiweke sawa halafu nianze shughuli rasimi kwani wale nilioua nje ilikua ni kasehemu kadogo ka majambazi waliomo ndani. Mara wakati najiandaa kwani kuna sehemu walikaa kikundi nikamwona mtu mwingine akija. Nikabana mlangoni na alipofika sikuuliza nilimtia kisu tumboni nikachomoa nikatia tena nikachomoa nikachoma mara ya tatu. Nilikua nimevurugwa kichwa kwakweli sikua na huruma na majambazi. Akaanguka nikamsachi kama anachochote ndipo niligundua alikua na silaha moja tuu bastola ndogo. Pia nikagundua alikua ni mwanamke. Wakati nainuka nisonge mbele nikasikia_____________________
EmoticonEmoticon