Zaidi
ya wakazi 180 wa kijiji cha mbugani wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza
hawana makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa na kimbunga kilichoambana na
mvua kubwa, ambayo pia imeharibu mashamba ya zao la muhogo pamoja na
miundombinu ya umeme na barabara.
Jumla ya kaya 33 za vitongoji viwili vya mbugani na CCM katika
kijiji hicho zimeathirika kutokana na kimbunga hicho ambapo familia za
waathirika kwa sasa zimepatiwa hifadhi ya muda katika nyumba ya diwani
wa kata ya bulyaheke bageti nyuti, huku wahusika wakiiomba serikali
kuwasaidia mahema pamoja na mablanketi ili kujisitiri na hali ya baridi
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kufuatia tukio hilo uongozi wa serikali ya wilayani Sengerema
umeanza kutoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa ajili ya waathirika hao,
hatua ambayo imeungwa mkono na watu mbalimbali akiwemo mkazi wa
Sengerema Eston Kasika ambaye ametoa kilo 1320 za unga wa sembe, kilo
460 za mchele, kilo 360 za maharage, lita 40 za mafuta ya kula, katoni
sita za sabuni za kufuli na katoni moja za sabuni za dawa, kilo 66 za
sukari, katoni mbili za chumvi pamoja na dazani 40 za maji makubwa ya
kunywa – vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne.
Afisa mtendaji wa kata ya bulyaheke mabula Enock amesema tathimini
ya nyumba zilizoezuliwa iliyofanywa na wataalamu wa halmashauri ya
wilaya ya Sengerema ni zaidi ya shilingi milioni.
EmoticonEmoticon