Chama cha demokrasia na maendeleo -CHADEMA- kimesema hakitakubali serikali ya awamu ya nne kuongezewa muda wa kukaa madarakani kutokana na kusuasua kwa zoezi la uandikishwa wa daftari la wapiga kura.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
viongozi wa chama hicho wa ngazi ya shina hadi wilaya wa mkoa wa Dar es
salaam, mwenyekiti wa Chadema taifa ameitaka serikali kuharakisha zoezi
la uandikishaji wapiga kura na kusisitiza tarehe ya kupiga kura katika
uchaguzi mkuu wa mwaka huu ilijulikana nchi nzima kutokana kuwepo
kikatiba na kisheria kuwa ni jumapili ya mwisho wa mwezi wa 10.
Awali wakizungumza na mamia ya viongzoi wa chama hicho katika
mkutano huo naibu katibu mkuu wa chadema Zanzibar Bwana Salum Mwalimu
amesema lengo la chama hicho kuwa na viongozi wenye weledi na uwezo wa
kufanya kazi,huku naibu katibu mkuu wa chama hicho Tanzania bara Mhe.
John Mnyika amesema mafunzo hayo yataendeshwa nchi nzima ambapo
yanatarajiwa kuwafikia viongozi wa chama zaidi ya laki 2 na ishirini na
nne elfu.
EmoticonEmoticon