TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 15.04.2015.





·   MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA SHIWANGA AUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.


·   JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA MANYANYA WILAYANI CHUNYA AKIWA NA POMBE MOSHI UJAZO WA LITA 05.
 

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MWANAMKE MMOJA MWENYE UMRI WA MIAKA 60 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ESTER LONDON MKAZI WA KIJIJI CHA SHIWANGA WILAYANI MBOZI ALIFARIKI DUNIA AKIWA NYUMBANI KWAKE KUTOKANA NA MAJERAHA ALIYOYAPATA BAADA YA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

INADAIWA KUWA, MNAMO TAREHE 01.04.2015 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHIWANGA, KATA YA IGAMBA, TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA, MAREHEMU AKIWA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI KIJIJINI HAPO ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA NDIPO ALIPELEKWA HOSPITALI YA MBOZI MISHENI KWA MATIBABU KISHA KURUDI NYUMBANI 13.04.2015. 

HALI YA ESTER LONDON ILIBADILIKA NA ALIFARIKI DUNIA MNAMO TAREHE 14.04.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI. CHANZO CHA TUKIO HILI NI KIPIGO KILICHOTOKANA NA IMANI ZA KISHRIKINA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI MBOZI. UCHUNGUZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
                                                                                                                                        
KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA MANYANYA WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ESTER ATHUMAN (48) AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05] NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO HARAMU.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.04.2015 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA MANYANYA, KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHIN KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UPIKAJI/USAMBAZAJI NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Previous
Next Post »