SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHULUA SURA YANGU? SEHEMU YA TANO



MTUNZI NA MWANDISHI-MWL.YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/Watsap,Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email, yusuphngahala@gmail.com, Instagram@mwalim_yuu.

SEHEMU YA TANO.
             Tulipoishia Nikaona "Yes" nimemwona mbaya wangu. Nikaegesha gari pembeni nikashuka na kuanza kumfukuzia kwa nyuma. Nilipomkaribia mara ghafla____Songa nayo........Kuna Lori kubwa la contena mbili likawa linapiga honi. Ilinibidi bisimame kusubiri lipite. Likawa limetutenganisha na yule mtu. Nilipata shauku hata ya kuruka lile gari kwani niliona linanichelewesha. Baada ya kuisha nikavuka na kupepesa macho sikumwona mtu. Nililaani sana lile lori nikaona limenikwamisha mambo ya maana. Nikaamua kurudi kwenye gari. Baada ya kufika nikafungua mlango na kuingia.

            Nilishtuka kwenye siti yangu naona kitu cha ajabu kidogo. Niliona bunduki aina ya SMG, Sikua nimeiweka mimi. Hata hivyo mimi sina umiliki wa bunduki ya aina hiyo. Nilishtuka sana. Nikaangalia siti za nyuma sikumwona mtu. Nikatoka na kuangalia nje labda nitaona kitu lakini wapi. Nilishtuka na kujisemea moyoni Hakika tumezidiwa na wajanja. Nikavaa "groves" na kuichukua na kuiweka siti za nyuma baada ya kuihakiki ya kua iko salama. Nikawasha gari na kurudi kituoni. Nilipofika nikamwita Juma na Peris nikawaambia yale yote kisha nikamwomba Juma anisaidie kitu. Nilimwomba anisaidie kupata taarifa kamili za huyu mtu anayeitwa Zabroni Makweka.  Nikamwambia nahitaji kufikia jumatatu niwe najua ni nani mimi pia namfuatilia sana tuu. Leo nilihisi kuna mahali nilimwona ila nikashindwa kumtia nguvuni.

                      Bila kinyongo Juma alikubali. Baada ya hapo nikaendelea na upekuzi wangu juu ya Zabroni Makweka. Niligundua mambo mengi sana juu yake. Niligundua kuna kesi zisizopungua 21 za ujambazi ameshiriki moja kwa moja. Ushahidi wa picha katika kila tukio ulikuwepo. Kilichokua kikinichanganya ni kua picha zote ninazoziona ni Sura yangu labisaa hakuna tofauti yoyote. Nilikua najiuliza hiki ni nini jamani? Au ni uchawi? Hapana hadi kompyuta zishimdwe kugundua! Hapa kuna kitu. Nikafanya upekuzi sana nikajua pia alishawahi kuua viongozi kadhaa wa serikali ya Tanzania.

              Huyu Zabroni ni nani? Akili ilikua imesimama. Nikaamua kurudi nyumbani. nikiwa njiani simu yangu ikaingiza ujumbe mfupi wa maneno yani SMS. Sikutaka kuisoa kwasababu nilikua barabarani. Niliogopa sana ajali. Nilipofika nyumbani wakati napaki gari kuna mtu alitoka mbio toka ndani mwangu. Nilishuka haraka na kuanza kumfukuzia. Alikua anakimbia haswaa. Alinizidi na kutokomea zake. Nikaamua kurudi nyumbani nikaangalie hali ya ndani Nilipofika nikakuta vitu vimesambaa sana sebuleni. Nikaingia chumbani na kumkuta mke wangu amefungwa. Nikamfungua na pia mwanangu alikua kafungwa. Niliwafungua wote Nikashangaa yule mtoto wa marehemu bosi wangu anavuja damu mdomoni.

              Nikamfuata na kumuuliza shida nini? Alikua akilia tuu. Mke wangu akasema Mume wangu huyo mtoto wamemkata ulimi. Nilishtuka na kuuliza unasema? Akajibu ndo hivo amekatwa ulimi mbele ya macho yangu. Nikauliza ni nani aliyemkata? Akajibu sasa mi nitamfahamia wapi? Simjui hata sijawahi kumwona ni sura ngeni. Nilimwambia mke wangu tumkimbize hospitali mara moja. Tulitoka na kuwahi hospitalini. Baada ya kufika madaktari walimhudumia vizuri sana. Baada ya mda wakaniita wakanambia unaweza kurudi naye nyumbani lakini hatoweza kuongea kamwe. Nilipigwa na butwaa. Nikasema dokta hakuna hata jinsi ya kufanya akaweza hata kusema maneno kiasi. Akajibu haiwezekani pia tumegundua kitu kingine inaonekana amewekewa sumu masikioni. Hatakua na uwezo wa kusikia pia.

                   Nilijikuta napagawa kwanini dokta kwanini? Akajibu pole mkuu. Nikasema kwa gadhabu kuu hivi ni kwanini wanamwandama mtoto? Hana hatia hana kosa lolote! kwanini wanamharibia maisha? Niligadhabika sana kwa kile kitendo. Nikamchukua  mgonjwa na kwenda nyumbani. Nilifura kwa hasira. Mke wangu alikua yuko kimya kwasababu ananijua nik iwa na hasira hua siongei. Tulipofika nikamshusha yule mtoto. Huruma ilinitawala Nikakumbuka kuna ujumbe uliingia nikiwa barabarani na sikuusoma.

               Nikatoa simu na kuifungua ndipo nilipokutana na ujumbe huu. "NASIKIA UNAFUATILIA FAILI LANGU ACHA MARA MOJA KWA LEO NAKUONYESHA TRELA NYUMBANI KWAKO By ZABRONI" Nilishtuka sana nikaangalia namba iliyotuma sikuona namba. Aaah sasa hii mana yake nini jamani. Afisa natishiwa maisha kweli. Niligadhabika nikasema moyoni Lazima Zabroni nikutie nguvuni.

                Nilipumzika mle ndani usiku ukaingia na siku kama mbili au tatu hivi zilikatika. Nakumbuka ilikua Jumapili nikiwa nimetoka kanisani nikaamua kwenda kumwona Juma. Nilikua na gari langu majira ya saa sita na nusu mchana. Nilitoka ibada ya pili. Baada ya kufika kwa Juma getini nilimwona mdada mmoja amevaa hijabu na juba jeusi. Alinisalimia mambo nikajibu safi. Akapita na kwenda zake. Nilijua katoka kwa Juma kwani Juma alikua anapenda sana "totozi" Basi nikasonga hadi ndani.

               Nilikuta mlango uko wazi. Nikapiga hodi mara kadhaa bila majibu.Nikaamua kuingia baada ya kufika sebuleni nikakuta Juma akiwa na kisu tumboni. Baada ya kusogea nikgundua kichwa chake kimekatwa na kipo chini. Ni uuaji sawa na ule niliyokutana nao kwa mkuu wangu wa kazi. Nikatoka haraka ili nimwone yule msichana. Lakini kwa bahati mbaya sikmwona. Nilirudi ndani na nikaingia chumbani kwa Juma. Nikakutana na kikaratasi kimeandikwa___________________

___________________________________________________________________________________________________________Jiunge na mwalimu sehemu ya 6 ujue yaliyojiri. Pia fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala kuna simulizi nyingi nzuri kama hizi niadd twende sawa. Nawapenda wote Popote mlipo Mungu atubariki sote.
Previous
Next Post »