SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?SEHEMU YA 12

Displaying 20150422_131147-BlendCollage.jpgMTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com, fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala. Instagram/mwalim_yuu.

SEHEMU YA KUMI NA MBILI.
Tulipoishia Wakati naendelea kukagua miili ya maaskari kuna ujumbe uliingia kwenye simu yangu. Niliitoa na kuangalia nani mtumaji. Chaajabu ni kua sikua "nimesave" namba ya Zabroni lakini jina lilitokeza Zabroni. Nilishtuka sana nikaufungua nao ulisomeka hiviii_____songa nayo......MJINI AKILI NYINGI JIPANGE AFANDE YUU. Nilipiga kichwa kwa gadhabu na kuona niliyezidiwa akili na watoto wa mjini. Wakati nataka kujibu ule ujumbe namba haikuwepo yani jina lilitokeza sawa na vile, Tigo, au voda wakituma SMS, huwezi kujibu na jina unaliona. Nilishangaa sana. Haikua nacheza na mtu wa kawaida sana. Nikaamuru majeruhi wakimbizwe hospitalini mara moja.

Roho yangu iliumia sana kupoteza nafsi zisizo na hatia. Nilimlaani sana Zabroni lakini sikua na jinsi. Nilitoka pale nje nikaingia ndani na kutafakari nikaona njia pekee ni kumfuatilia kwa siri. Nikapanga mipango kadhaa kisha nikaona inafaa. Miongoni mwa mipango yangu ilikua niteue maaskari wasiopungua wanne kisha tumfuatilie kwa siri. Baada ya mda nilitoka nje na kuona tayari zile maiti za maaskari wenzetu zimepelekwa mochwari. Ili kusubiri ndugu na jamaa kuja kuchukua zile maiti. Nakumbuka Peris alikua ametangulia na Anthony nyumbani. Baada ya taratibu zote kukamilika na baadhi ya ndugu kuchukua maiti za wapendwa wao. Tuliwapa vikosi vya kuwasindikiza msibani.

Usiku ukaanza kuchukua nafasi yake taratibu. Niliamua kwenda nyumbani ambapo nilitoka ofisini mida ya saa mbili usiku. Niliendesha gari langu huku nikiwa na mawazo sana. Nikafika nyumbani na kukuta Peris ameandaa kila kitu. Niliwakuta wamekaa sebuleni na Anthony wakicheza michezo mbalimbali. Baada ya kuingia ndani na kubadili nguo nilitoka Peris akaandaa chakula na yeye pia kukaa ili tule. Nikashangaa na kuamua kumwuliza. Ulikua hujala? Akajibu ndio nilimwandalia Anthony tuu mimi nilikua nakusubiri wewe. Moyo ulilipuka paah!! kwa furaha. Nikamwambia ahsante sana kwa kunijali Afande. Mara akabadilika usoni akaonekana kukasirika. Nilijua ni kwasababu nimemwita jina la afande.

Nikamwambia natania jamani Peris wangu. Kusikia vile akafurahi kidogo kisha tukala. Alikua akinilisha mara kwa mara. Alinikumbusha maisha ya ndoa na mke wangu kipenzi. Wakati tunaendelea kula mara simu yangu ikaita. Nikaipokea na kusikia kuna watu wako pale hospitalini wanataka kumwua mkuu wa kituo. Nilipata woga kiasi kisha nikawambia "okey" nakuja nikamwambia Peris hebu mwangalie Anthony hapa narudi. Nikaingia chumbani na kuvaa nguo za kazi kisha nikaanza safari. Nikiwa njiani nilihisi kitu. Kwanza kuna gari ilikua mbele yangu niliitilia shaka kua ni maadui.

Pia gari ya nyuma nilikua nishagundua kua si watu wema. Nilikua nimezingirwa kifupi. Nilitamani kuwapita lakini ilishindikana. Mara yule wa mbele akasimamisha gari kwa ghafla. Kwakua nilikua jirani sana na ilikua ghafla hivyo nikamgonga kwa nyuma. Nilijigonga kwenye usukani na vioo vilivyopasuka vikanichoma sana usoni na kichwani. Lile gari la nyuma likasimama. Na mbele wakashuka watu wawili mbele. Na wawili nyuma. Sikua nawaona vizuri kutokana na maumivu.

Walikuja dirishani na kisha wakapasua kioo cha dirisha. Walikua wamevalia suti nyeusi. Kisha wakatoa chupa fulani. Wakaifungua na kunimwagia. Nilihisi kama mtu anakata ngozi na kiwembe kikali mno. Niliinua kichwa na kuwaangalia wakanimwagia usoni kwa uzuri. Nilikua kama ninayehisi maumivu ya moto mkali sani. Kisha wakatoweka. Sikujua nini kiliendelea hadi hapo niliposhtuka nikiwa hospitalini. Nilikua nimezungukwa na madaktari wengi sana. Swali la kwanza nikauliza mkuu yuko wapi? Nikajibiwa tulia kwanza vipi hali yako? Aliuliza daktari mmoja. Nikamjibu sielewi mke wangu yuko wapi?

Nilikua naongea vitu visivyoeleweka Ba asi wakasema ebu lala tena upumzike. Nikasikia na kulala.Nilikuja kuzinduka tena baadae hapo akili ikawa imerudi sawasawa. Nikaanza kuhisi maumivu makali usoni na kifuani. Nilipotaka kujigusa nikaona nimezungukwa na bandeji uso mzima. Nilikua naumia sana. Nilikaa pale kwa siku mbili huku Peris akiwa karibu sana. Chaajabu ni kua sikua naona maaskari wengine kuja.

Sikulijali hilo lakini nilishangaa siku ile Peris anakuja na gezeti fulani la udaku maarufu sana hapa Tanzania. Alikua kama mwenye huzuni fulani. Basi alipofika akanipa lile gazeti na kusema soma hapo Yuu. Nililipokea na kusoma ukurasa wa mbele. Ukurasa ulipambwa kwa picha zangu mbalimbali na maandishi yaliyokolezwa wino wa njano. Yalisomeka hivii. "AFISA POLISI AKUTWA AKIBAKA WANAWAKE KANISANI". " ATUMIA BUNDUKI KUWATISHIA" "WANANCHI WAMFUMA KUMKATAKATA MAPANGA" Kisha zikaonyeshwa picha nikiwa na bandeji. Zaidi pale zilionyesha nikiwa uchi nabaka wanawake kanisani. Kiukweli picha zilikua ni zangu lakini mbona mimi nilikua hospitali. Majibu ya daktari ni kua nilimwagiwa tindikali hatari sana sasa hili la kubaka limetokea wapi jamani mbona sielewi.

Hali yangu ilikua si nzuri sana. Niliumia sana kuona naandikwa vitu visivyo vya kweli. Nilitamani kuinuka na kumfuata mwandishi nimtie adabu lakini ningetokaje tayari nina tindikali mwilini. Wakati natafakari nifanye nini akaingia daktari ambaye alikua kavaa kofia iliyomziba uso asionekane. Akamwambia Peris naomba nipishe mara moja. Akatoka na alipotoka yule daktari akaandaa sindano yenye dawa kisha akanisogelea karibu. Mara akaniziba mdomo kisha akatoa kofia. Mungu wangu sikuamini ninachokiona. Pia nilipoangalia sindano kwenye bomba mle ile dawa niliyoiona kwa uzoefu niligundua ni sumu. Mara taratibu akaanza kuisogeza akitaka kunichoma.

Sura yake ilikua inafanana sawasawa na yangu. Mpaka nilijihisi najiangalia kwenye kioo. Hakika nilikua ni mimi. Akaanza kujiongelesha pale. Mimi ndiyo Zabroni Makweka hakuna polisi aliyewahi kunishinda. Hii ni sindano ya sumu kali sana unakufa ndani ya dakika kumi. Nakuchoma sasa unaleta vikwazo mjini hapa. Akanidunga ile sindano mkononi. Akamaliza na kuichomoa kisha akavaa kofia na kuondoka zake. Hakika nilizidiwa ujanja. Nilianza kuhisi mabadiliko ya mwili palepale. kwani nilihisi______________________

__________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Je nini kilijiri? kutana nami sehemu ya 13, Kwa lolote nichek kwa inbox fb.com/Mwalimu Yusuph amAbel Ng'ahala. Au Email@yusuphngahala@gmail.com. au sim no,0755683295 na Instagram @mwalim_yuu. Nawapenda sana siku njema wote.
Previous
Next Post »