https://igcdn-photos-g-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xaf1/t51.2885-15/11189319_717166851727526_1611832119_n.jpgAMBER ROSE AELEZEA NIA YA KURUDIANA NA ‘KIPENZI CHAKE’ WIZ KHALIFA
MWANAMITINDO maarufu wa Marekani, Amber Rose, ameelezea nia yake ya kurudiana na mzazi mwenzake, mwanamuziki Wiz Khalifa ambaye walizaa naye mtoto mmoja na kuachana mwaka jana baada ya kuishi pamoja kwa mwaka mmoja tu.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 31 amemwelezea Khalifa kama ‘Pendo la Maisha Yangu’ na kwamba anafikiria suluhu itapatikana.

Akihojiwa na gazeti la Mail kwa njia ya mtandao, Rose ambaye ana mtoto mmoja hadi sasa alisema: ''Hatujarudiana, japokuwa napenda iwe hivyo. Yeye ni pendo la maisha yangu ambaye tuna mtoto naye, japokuwa sasa tuna mahusiano na watu wengine. “Tunataka kurudisha urafiki wetu wakati tunashirikiana kumlea Sebastian, jambo ambalo ni muhimu zaidi kwetu.” Alisema Amber
Previous
Next Post »