SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 9

Displaying 20150418_100633-BlendCollage.jpg
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com. Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala,. Instagram@mwalim_yuu.

SEHEMU YA TISA.
            Tulipoishia Amekimbizwa hospitalini. Nilishtuka nikampigia na kumwuliza nani kampiga akajibu ni watu wssiojulikana. nikakata simu. Mara simu ya peris nayo ikaita. Alipoangalia namba ikawa namba yake ndo inampigia. Alishtuka sana. Nikamwambia Peris_____Endelea...... Pokea usiogope ni hawa hawa wanaharamu. Peris akasema Afande hivi ni kwanini hali inakua hivi? Nikajibu hapa kwakweli jeshi letu inabidi kujipanga kwasababu kuna mawaziri mpaka viongozi wakubwa wa kiserikali. Wanahusika na mtandao huu na wanawatuma hawa sasa sijui kama tutafanikiwa. Kawani tunashindana na serikali sasa na si majambazi tena. Wanatishia maisha yetu wanatoa rushwa kwakweli Mungu atutie nguvu.

                   Wakati wote tunaongea simu ilikua bado inaita. Mpaka nilishangaa simu gani isiyokatika. Peris akaipokea na kuweka "loud speaker" ikasikika sauti ikisema Najua uko na Afande Yuu mko kwenye foleni Mwenge. Sasa tunawaonya kaeni mbali na sisi mtapoteza maisha mkikaidi. Nilipatwa na hasira na kuona tunachezewa akili. Nikajibu kwa nguvu Tutawakamata na tutawapeleka mahakamani. Mara simu ikakatika. Tulibadili safari badala ya kwenda nyumbani tukawa tunaenda hospitalini kumwona Anthony anaendeleaje!

              Tulifika hospitalini tukapokelewa kisha tukaelekezwa wodi. Tulielekea wodini lakini ghafla tulipofika mlangoni tulipishana na mtu aliyekua amevaa kama daktari akitoka. Kilichonishtua ni kua mtu yule alikua na wasiwasi sana. Alionekana kama mwenye haraka na anayekwepa kitu.Nikamtilia shaka nikaamua kumkamata. Baada ya kuona nimemkamata alichukua vidonge fulani akameza. Nilijitahidi kumzuia asimeze ilishindikana. Haikuchukua hata sekunde ishirini alianguka na kupoteza maisha. Hii ni njia ya majambazi kulindana. Hua wanakwepa kuhojiwa hivyo huona bora afe kutetea wengine.

                  Swali ikawa je ametoka ndani kufanya nini? Nikaona nimwite daktari haraka amfanyie uchunguzi mtoto. Mara baada ya kumchunguza akasema amechomwa sindano ya sumu. Aaashi!! Nilijikuta natamka kwa mshangao. Kwanini huyu mtoto jamani? Aliuliza Peris, Nikajibu hata mimi sijui kakosa nini kila wakati wanajaribu kumwua jamani. Daktari akajibu naombeni tumshughulikie kwanza halafu mtamwona hii sumu ni kali la sivyo tutamkosa mtoto.

                Tukatoka nje na kukaa mda ukasonga. Baada ya kitambo kirefu daktari akaja na kusema anaendelea vizuri ila hatutaruhusiwa kumwona mpaka kesho yake. Nilimbembeleza daktari na kumwambia kua yule ndie mtu pekee anaenifanya nifarijike. Daktari akajibu sawa najua ila kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari pole sana. Nikaamua kumweliewa daktari na kuondoka. Tulifika Nyumbani kwangu na Peris akapika tukala. Tulikua na furaha kiasi. Furaha yetu ilikua imechukuliwa na majambazi na mauaji.

            Mda ulikua umekwenda sana ilikua saa 4:35 usiku, Peris akaomba nimsindikize kwake akapumzike. Kwakua tulikua tunakaa jirani haikua tabu. Tukatoka na kuwasha gari kumpeleka Peris kwake. Tulifika kwa Perisi na kushuka. Lakini tuliposhuka kuna kitu tofauti Perisi alihisi. Kwanza alisema taa ya ndani inawaka na yeye alizima. Wakati namwambia akumbuke vizuri mara kikaonekana kivuli cha mtu mle ndani akikatisha mara huku mara kule.

              Ghafla alikua kama aliyehisi kitu akafunua pazia na kutuchungulia. Alipotuonau akafunika pazia kisha akazima taa. Pale ikawa ngumu hata kuingia kwani hatukujua yupo chumba gani, Zaidi wako wangapi? pia na silaha gani? Nikamwambia Peris hapa kilichobaki ni kujitoa mhanga kama ni kufa acha tufe tukitetea taifa letu. Mimi naingia alidakia Peris aliyekua na wazo kama langu. Basi wakati tunaongea mara taa ya chumba kingine ikawashwa. Kisha ikazimwa tena.

               Ikawa kama mchezo. mara taa ziwashwe zote mara zizimwe. Nikamwambia Peris sasa tufanye hivi mmoja azunguke dirisha la nyuma na mwingine mbele kisha. Tuamshe mashambulizi. Akajibu sawa lakini wakati anasema vile mi nikamwona mtu anaruka ukuta na kutokea kwa nje. Sikukubali na mimi nikakimbilia ukuta na kuruka. Kwa bahati mbaya nilikua nimechelewa. Yule mtu alikua na pikipiki yake aliipaki kule na akawa tayari anaishia zake na kuniachia vumbi.

                Nililaumu sana lakini kukawa hakuna namna. Nikarudi nikamwambia Peris ya kua yule mtu alikua mmoja. Tukaamua kua liwalo na liwe tunaingia ndani. Tuliandaa bastola zetu na kujiweka sawa kisha tukavamia ndani. Kulikua kumesambazwa makablasha kibao ya Peris yule mtu alionekana kuna kitu alikua anapekua. Hapakua na dalili ya mtu yeyote kuwepo. Baada ya kuhakikisha usalama kwa kiasi fulani tuliweka bastola vizuri kisha tukaanza kuangalia mle ndani labda tungeona chochote. Tulipekua na kupesapesa macho lakini hatukuona kitu.

                   Tukiwa pale Peris akasema Afande siwezi kulala humu peke yangu. Nikamjibu kwahiyo itakuwaje tunarudi wote? akajibu ndiyo au tulale hapa wote. Wakati nafikiria nimjibu nini juu ya oazia la chumbani kwake nilihisi kuna kitu kinang'aa nikaenda kukichukua. Kilikua kidogo sana kwakweli lakini kwa uzoefu ilikua ni kamera yenye nguvu sana. Pia nikaona kwenye mto wake kuna viashiria vya kitu nikaugeuza na kukutana na kinasa sauti kidogo pia. Nikamwambia Peris, Hapa tuna kazi ya ziada kwani hawa wanaonekana wamejitosheleza. Wakati peris anataka kujibu mara tukasikia_____________________

_______________________________________________________________________________________________________________________________________Kutana nami sehemu ya 10, Pia nitembelee fb kwa simulizi zaidi, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com,Instagram@mwalim_yuu na Watsap ni 0755683295. Byebye love u all.
Sent from Huawei Mobile
Previous
Next Post »