SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 10

Displaying 20150419_142647-BlendCollage.jpg

MTUNZI NA MWANDISHI-MWL-YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/Watsap,Fb.com/
Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com, Instagram @mwalim_yuu.

SEHEMU YA KUMI.
Tulipoishia Pia nikaona kwenye mto wake kuna viashiria vya kitu nikaugeuza na kukutana na kinasa sauti kidogo pia. Nikamwambia Peris, Hapa tuna kazi ya ziada kwani hawa wanaonekana wamejitosheleza. Wakati peris anataka kujibu mara tukasikia______Songa sasa...... Simu ya Peris inaita akaichukua na kuiangalia, akasema hii namba ngeni afande. Nikamjibu pokea tuu. Akaipokea na kuweka "loud speaker" Mara ikasikika sauti ikisema Hivi baby kwanini simu zangu hupokei? Mpaka nakupigia kwa namba ngeni kweli? "Come on" Peris nisamehe nilishakwambia shetani............ Mara Peris ajakunja uso na kukata simu kwa hasira. Kwakua nilimwona ana hasira sikutaka kumwuliza ana shida gani nikamwacha. Nadhani pia hakutaka nisikie maongezi yake ila ni kwasababu tulihisi huenda ni wale wanaharamu.

Basi tuliendelea kupekua mle ndani na hatuluona kimgine. Ila Peris alidai kua baadhi ya nyaraka muhimu za kipolisi hazioni. Hii inamana ziliibwa na yule bwege aliyetoka mle. Kwakua tulishakubaliana atakuja kulala kwangu safari ikaanza kurudi kwangu. Tulifika kwangu na kuingia ndani mda ulikua umesonga sana ilikua ni saa saba kasoro usiku. Wote tulikua tumechoka sana. Peris akaingia chumba cha wageni na mimi nikalala chumbani kwangu. Nilikua nikimfikiria mke wangu sana.

Niliumia sana kumkosa mke wangu. Asubuhi Peris alikua wa kwanza kuamka na akafanya shuhuli zote za ndani na nje. Aliosha vyombo, akadeki akafagia uwanja. Na zaidi akaandaa maji ya kuoga na kunyoosha nguo zetu wote. Kisha akaja kuniamsha chumbani kwangu. Alikuja amevaa khanga moja tuu ambapo aliniita jina langu halisi. Yuu... Yuu! amka mda unaenda. Aaah nilishtuka nikamwambia aaah Peris ni wewe nilikua naota mama! Nikajinyoosha na kupiga mwayo. Kisha nikamwangalia vizuri huku nikifikicha macho kutoa tongotongo.

Mashaallah Peris, Alikua amekaa pale kitandani khanga ikaachia sehemu kubwa ya paja. Macho hayana pazia nilijikuta nakodolea macho pale hadi alishtuka. Akasimama na kusema inuka basi ukaoge ujue inabidi tupitie hospitali kwa Anthony. Kisha tuwahi ofisini hebu inuka Yuu. Hali ile ilinikumbusha mke wangu ambapo alikua akiniamsha kuwahi kazini. Perisi akawa anatoka anaelekea sebuleni. Sijui alikua anafanya makusudi maana huo mtikisiko niliouona Mungu wangu. Hakika alikua amejaaliwa haswaa. Alikua na umbo zuri sana kwakweli. Nilimwangalia mpaka alipopotea.

Niliamka na kuelekea kuoga. Baada ya kuoga nilitoka naye Peris akaingia kuoga. Wakati anatoka nilikua niko sebuleni najiandaa kiasi. Akapita na khanga imelowana Woyii!!! Roho yangu ililipuka paa!! Uchu wa mapenzi ukanijaa ila nikajizuia. Baada ya kujiandaa tukaondoka hadi hospitalini. Peris alikua ndiye anaendesha gari. Tulifika na kuulizi maendeleo ya mtoto ambapo tukaambiwa kwa sasa amezinduka ila kuna watu walikua wanakuja hapa tulikua hatuwaelewi.

Inaonekana huyu mtoto anawindwa sana. Hivyo anahitaji ulinzi. Niliwasikiliza wakatuambia mambo mengi sana. Kisha tukaruhusiwa kumwona tukamwona lakini alikua bado yuko chini ya uangalizi maalumu. Tukaondoka na kuwahi ofisini baada ya kufika niliwakuta vijana wamejiandaa tayari kwa kufanya operation hawakujua kama tayari mpango wetu ulijulikana na majambazi. Nikawaita na kuwatarifu jinsi gani taarifa zetu ziliwafikia. Nikawaambia nahisi kuna usaliti.

Nikawaonya kua ikiwa kuna yeyote anayevujisha siri za jeshi tukimkamata huyo halali yetu. Basi nikawaambia tujipange upya ili tufanye mashambulio ya siri. Tulikubaliana na kutulia mimi nikaamua niendelee na upepelezi wa wale majambazi. Kwakua kila wakipiga simu namba zilikua zinakuja mpya au wakati mwingine namba yangu. Nikaamua kwenda mamlaka ya mawasiliano TCRA ili nikajue au kupata msaada. Nilifika huko na kuhudu iwa vizuri sana.

Nikaambiwa pia niende ofisi za mitandao ya simu kwaajili ya kuchukua taarifa za namba zile. Kwani kule nilipewa namba mbili ambazo ndizo hupiga. Nikatoka nikiwa njiani naelekea ofisi za Vodacom Tanzania. Simu yangu ikaita. Niliangalia alikua ni afande mwenzangu pale kazini baada ya kupokea nikasikia sauti ikisema. Madaktari wanne pamoja na Anthony wametekwa na watu wasiojulikana.

Moyo ulilipuka kwa mshangao. Nikapaki gari pembeni kisha nikasikiliza maelezo kwa kina. Nikaambiwa mahali wameelekea. Ilikua ni maeneo ya fukwe za koko. Bilimpigia simu hapohapo Peris na kumwambia aje na kikosi cha askari 20. Baada ya mda wakanambia tayari wanakaribia na mimi nikawasha gari kisha tukakutana huko. Tulianza kwa kulizingira eneo lile ambapo taarifa za kiintelijensia zilionyesha wapo. Tulikaa pale kwa mda.

Hatukuona chochote. Doria ilichukua mda sana mpaka tukaanza kukata tamaa. Hapakua na dalili hata ta mtu kupita wala kuonekana eneo lile. Wakati nazidi kuzunguka chini huku nikiwa nimelala. Mara kwa mbali nikaona kuna gari inapaki. Alishuka mtu mmoja ameshika bunduki. Nikawatarifu wenzangu kua makini. Yule mtu akawa anakuja mahali tulipo. Alisonga mpaka tukahakikisha yupo katikati. kisha nikatoa amri ya kumsogelea kwa karibu. Tulisogea kwa tahadhari ambapo yeye alikua hajashtuka bado. Wakati natoa amri ya kumshambulia ghafla yule mtu___________________________
_________________________________________________________________________________________________________________________Kutana na mimi sehemu ya 11 tuone kichojiri. Kwa lolote nichek 0755683295 au niinbox fb kwa jina Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.au Email@yusuphngahala@gmail.com. Au instagram@mwalim_yuu.
Sent from Huawei Mobile
Previous
Next Post »