SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?SIMULIZI SEHEMU YA 8


Displaying 20150417_130737-BlendCollage.jpg
MTUNZI NA MWANDIHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/Watsap, Email @yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Instagram @mwalim_yuu.

SEHEMU YA NANE.
             Tulipoishia Tulitoka Njombe mimi na Peris na Anthony yule mtoto wa marehemu bosi. Kichwani nilikua napanga kuua tuu na kuwapoteza wote na sitaacha hata mtu mmoja. Hakika nilikua nimegadhabika. Safari ya kurudi Dar es salaam ikaanza hivo.
******************************

*****
                Maisha ya Dar es salaam yaliendelea kama kawaida. Nilirudi ofisini na kuendelea na shughuli kama kawaida. Nilikua nafuatilia kesi za wale majambazi kwa ushirikiano na Peris. Nilianza kushughulika na Zabroni Makweka. Huyu ndiye alikua akiisumbua akili yangu kuliko majambazi wote. Sababu kubwa ni kua jina lilikua si langu lakini sura katika matukio yake  naonekana mimi. Hali ile iliniumiza sana kichwa. Pili amehusika na kifo cha rafiki yangu wa karibu Juma. Nilifanya upelelezi wa kina sana.

               Nililazimika kufuatilia vingine kwa siri kubwa. Kuna siku nilitoka ofisini kwasababu nilipigiwa simu na mtu mmoja niliyempa kazi ya kumfuatilia yule jamaa kimyakimya. Baada ya kwenda nilifika pale aliponambia tukutane na kumkuta. Akasema kaka nimekuita hapa ili............Kabla hajamaliza kuongea ulisikika mlio wa risasi. Nikiwa nimetaharuki  yule jamaa akaanguka chini. Masikini ya Mungu kumbe ndo alipigwa risasi. Nikamwacha pale nijaribu kuangalia huku na huko lakini sikuona kitu. Nilisononeka sana.

             Nikaamua kupiga simu kituoni kutoa taarifa za mauaji. Wakati nimekata simu yangu. Mara simu yangu ikaita. Ilikua namba ngeni nikaipokea na kusikia sauti nzito tena ya kibosile. Mtu mwenye pesa nyingi. Alisikika akisema  Habari yako kijana. Nikajibu salama naongea na nani? Akajibu bila shaka naongea na afande Yuu? Nikajibu naam mimi ndiye nikusaidie nini? Akajibu sihitaji msaada wowote ila nataka nikusaidie wewe. Mimi ni naibu waziri wa(.........) akataja, sitaisema kwasababu za kiusalama. Kisha akasema nakuomba kijana achana na mambo yasiyokuhusu utadharirika bure. Acha mchezo na Tanzania wewe. Nikaanza kushangaa nikamwuliza unamanisha nini mheshimiwa? Akajibu achana na Nurdini Chinjachinja, Achana na Jarome Singano na pia mwache Zabroni Makweka hawa ni vijana wetu. Kama ni kiasi cha pesa sema upewe.

              Nilijikuta naishiwa nguvu na kujiona najaribu kupambana kwa nguvu kumbe napambana na Viongozi. Niliumia nikakosa cha kujibu kwakweli. Roho ya ujasiri  nilipokumbuka maneno ya mke wangu. Zaidi nilipokumbuka Kiapo changu cha kulinda nchi. Nikapata ujasiri wa ajabu nikamjibu. Sihitaji hela yako ya dhuluma, Nitawakamata wote hata wewe ukiwemo utakamatwa tuu. Akasikika akisema shauri yako ilikua ni kukusaidia tuu.

                 Nikaona ananiletea kiwingu tuu. Nikakata simu na kuendelea na shughuli zingine. Wakati ule mwili umechukuliwa nikawa narudi ofisini. Wakati nafika ofisini nikakuta ofisini kwangu kuna bahasha. Nikaiangalia nikaona imeandikwa afande Yuu. Nikamua kuifungua na nilipofungua ndani nilikutana na santuri "CD" ikiwa imewekwa mle ndani.

             Nikaiangalia sikujua ya nini nikaamua kuiweka kwenye kompyuta. Nikaanza kuangalia ina nini. Macho yalinitoka nikiwa siamini ninachokiona. Kwani niliona mtu yule ni mimi. Hilo halikua jipya. jipya na kubwa kuliko ni kwamba nilikua naona yule mtu anafanya mapenzi ya jinsia moja. Nilishangaa sana. Sasa mimi nimewahi kuwa shoga wapi jamani. Nikiwa nashangaa mara simu ikaita nikaipokea nikasikia. Sasa ni hivi iyo cd baada ya wiki moja itakua sokoni. Kazi kwako unayetaka kuufia uafande.

             Simu ikakatika, nikajaribu kupiga lakini namba haikuonekana. Nikaona kazi yangu inaanza kua ngumu. Nikafikiria mara mbili nikaona sipati majibu. Nikaona hapa ni kuandaa kikosi cha uhakika na kuwakamata ndani ya siku moja. Sikuona namna nyingine zaidi ya kupambana. Nikaitisha kikao cha ghafla. Maafande walikusanyika pale nikawaambia kilichopo mbele yetu ni mapambano tuu hakuna kitu kingine. Wajiandae kwa vita kali siku ya pili waandae na silaha. Niliwasisitiza na kuwatajia maeneo tunayoshuku majambazi hao kujificha.

               Tulijadili mambo mengi sana. Kisha nikawaruhusu wakajiandae kwaajili ya siku inayofuata. Mimi nikajiandaa na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Kwa kua Peris alikua hana gari akaniomba lifti. Haikua tabu pia akasema angependa aje kunisaidia kupika kwani ananihurumia ninavyoteseka na Anthony. Nilimkubalia tukaanza safari. Nikiwa kwenye foleni simu yangu ikaita. Nikaitoa nabkuangalia nani anapiga. Namba ikaonyesha ya Peris. Nikashtuka nikamwuliza vipi mbona unanipigia simu? akajibu hapana Yuu mi sipigi simu! Nikamwambia hii namba ya nani? Akaiangalia kisha akasema Afande hata mi sielewi ila namba yangu. Nikaamua kuipokea. Kwakua foleni ilikua haisogei.

              Baada ya kupokea nilichokisikia ni maongezi tuliyotoka kuyajadili ofisini. Nilishtuka sana. Nikasikiliza yani kila kitu tulichoongea kilisikika bila kikosewa. Nilipigwa na butwaa. Mara sauti ikasikika ikisema kajipange upya sisi siyo rahisi kiasi hicho. Nikaanza kufikiria kua kuna usaliti ndani ya jeshi na kuhisi labda mtu alirekodi na kuwatumia. Nilijisikia mzito sana. Kichwa kilikua kimekakamaa kwa kubeba mawazo yasiyohesabika. Nilikua nacheza na mtandao hatari sana.

            Mara foleni ikaanza kusogea. Peris akaniuliza vipi afande? Mbona umekosa raha ghafla. Ile nataka kumjibu kuna ujumbe uliingia kwenye simu yangu. Nilipotoa simu na kuangalia alikua ni jirani yetu pale nyumbani. ujumbe wake ulisomeka kua. Anthony kapigwa na kitu kichwani anahofiwa kupoteza maisha. Amekimbizwa hospitalini. Nilishtuka nikampigia na kumwuliza nani kampiga akajibu ni watu wssiojulikana. nikakata simu. Mara simu ya peris nayo ikaita. Alipoangalia namba ikawa namba yake ndo inampigia. Alishtuka sana. Nikamwambia Peris_________________________
______________________________________________________________________________________________Tembelea ukurasa wa fb wa mwl kwa Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala upate simulizi zaidi na ufurahi. Kwa llt nichek 0755683295 au niinbox fb, au Email@yusuphngahala@gmail.com. Nawapenda sana.
Previous
Next Post »