SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA SITA


Displaying 20150415_120340-BlendCollage.jpg
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/Watsap, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email, yusuphngahala@gmail.com,

Instagram@mwalim_yuu..

SEHEMU YA SITA.
Tulipoishia Nikatoka haraka ili nimwone yule msichana. Lakini kwa bahati mbaya sikmwona. Nilirudi ndani na nikaingia chumbani kwa Juma. Nikakutana na kikaratasi kimeandikwa_____Songa nayo.....ZABRONI MAKWEKA. Aaaaah! "why" mbona muuaji huyu hatari hivi. Wakati nimepigwa na mshangao pale kuna ujumbe ukaingia kwenye simu yangu. Uliandikwa hivi "You next" Nilijikuta naogopa na kuingiwa na wasiwasi. Muuaji hatari yeye alipenda kujiita chinjachinja. Na kweli alikua chinjachinja haswaa. Nilianza kuona kazi ya uaskari ni ngumu. Na ni kweli ngumu fikiria kuhatarisha maisha yako mwenyewe. Sikua na ujanja kwani nilikula kiapo mwenyewe kua ningelitumikia taifa kwa uaminifu.

Nadhani huu ulikua wakati wangu wa kuonyesha jinsi gani naipenda nchi yangu. Sikujali wachache wanaofanya juhudi kuiharibu. Nilipiga simu kituoni na kuwataarifu kua Juma moja kati ya marafiki zangu wa kazi na nje ya kazi. Tulipendana na Juma tulikua tukifurahi pamoja. Eti leo kaaga dunia. Sikuaini hata kidogo. Wakati nasubiri difenda ifike nikawa najaribu kuangalia simu ya Juma kama kuna watu aliwasiliana nao kabla ya kifo kumkuta. Chaajabu sikuona chochote. Nilishangaa sana nikashuku huenda yule muhalifu alifuta kila kitu kupoteza ushahidi. Mara nikasikia honi inapigwa nikajua maaskari wamefika nikatoka na kuwakuta. Wakaingia na kuubeba mwili wa Juma. Baada ya kufika kituoni kamati ikakaa na kunichagua mimi niende msibani kama msindikizaji toka jeshi la polisi. Pia Peris naye akajumuishwa hapo.

Juma alikua ni mtu wa Mara huko. Basi tukaambiwa tuna siku kumi tuu. Mwili ukafayiwa taratibu zote na kuusafirisha hadi Mara. Huko tulimpumzisha Juma ndani ya nyumba yake ya milele. Baada ya wiki Tukakubaliana na Peris turudi. Tulianza safari toka Mara kurudi Dar es salaam. Baada ya kufika ilitubidi kuripoti kwanza ili kama kuna lolote jeshi litambue uwepo wetu. Wakati tunafika ofisini tukabiwa tumeletewa mkuu mpya kutoma Mtwara. Tulionana naye na kuongea mengi sana. Alituruhusu kuondoka na kurudi nyumbani kisha turudi ofisini baada ya kumaliza likizo fupi iliyotokana na msiba wa kipenzi chetu Juma.

Nilianza safari ya kurudi nyumbani na nilipofika. Mke wangu alifurahi sana alinikimbilia na kunibusu mara kadhaa. Nilimbusu pia kisha akanikaribisha kwa kunipa pole. Nilimshukuru kisha nikawa nawaangalia wanangu yaani mwanangu halisi na yule mtoto wa marehemu bosi wangu. Nilimhurumia sana yule mtoto kwani alitiwa uziwi na ububu na wabaya wasiopenda nchi na watu wake. Nikawa sina jinsi zaidi ya kukubali matokeo. Japo nilikua na hasira sana juu ya kitendo kile. Mda ukasonga ikafika saa mbili usiku tukawa tunaangalia taarifa ya habari ya "TBC1" Huku nikiwa nimelala juu ya kifua cha mke wangu. Nilimpenda sana mke wangu alikua ni kila kitu katika maisha yangu. Sikupenda nimkose hata kidogo. Yalikua ni mapenzi haswaa. Basi tukiwa tunatazama mara tukasikia habari moja ikatushtua sana. Ilikua si nzuri sana.

Ilisikika ikisema, "Afisa mmoja wa upelelezi wa jini Dar es salaam mwenye namba za usajili___________Akutwa akiua watu na kubaka wanawake ovyo. Ikiwa TV inaendelea kuongea chaajabu ni kua Picha zilizokua zinaonekana ni zangu. Nilishtuka sana. Mke wangu alianza kusononeka sana. Niliinuka huku nikikosa cha kusema. Nikiwa nimeduwaa pale mara nikasikia simu yangu inaita. Alikua ni Peris nikapokea nikasikia Angalia "STAR TV" Akakata simu. Nikabadili Chaneli ambapo nikakuta ile taarifa ya kua mimi nimekutwa naua na kubaka inaanza. Kichwa kikazidiwa kwa mawazo.

Mke wangu akasikika akisema mume wangu. Hapa kuna kitu si bure kwanini kila siku wewe tuu? Kwa kua nilikua na hasira nikamjibu kwa gadhabu. Kwahiyo unahisi mimi nayafanya hayo au? Akajibu hapana ni kwasababu naona mazi ngira ya wewe kusingiziwa kabsaa. Wewe hukuwepo ulikua safarini kwahiyo huko kubaka na kuua umeua msibani? Nikajibu hata mimi nashangaa jamani. Tukiwa tunaongea mara nikasikia mlio wa gari. Kwa uzoefu wa "diffender" za polisi nilijua tuu ni yenyewe. Mara mlango ukagongwa nikainuka na kwenda kufungua wakaingia maafande wawili. Mkuu unaombwa ofisini mda huu.

Sikua na jinsi pamoja na uchovu wa safari nikaungana nao. Baada ya kufika kituoni ilikua mida ya saa tatu usiku. Nakumbuka bosi akaniita kwa mahojiano mafupi. Ilikua ni juu ya Tukio lile. Baada ya kumwelekeza juu ya mlolongo mzima mimi na huyo mtu asiyejulikana. Baada ya kumwelezea kua mimi nilikua msibani na siku ya tukio ndo tulikua safarini tukirudi. Nikampa na tiketi zetu pamoja na ya Perisi. Basi akaonekana kua mpole kiasi kisha akasema sasa kama askari umeshindwa kumkamata huyo mtu? Nikajibu wili iliyopita ndipo nilianza kumfuatilia na Juma ndipo Juma aliuawa. Nadhani nitaendelea kesho kutwa. Akajibu sawa Afande ila Nitakuhitaji tena kesho kwa mahojiano zaidi.

Nikamjibu sawa. Akasema kesho nitaita vyombo vya habari kukanusha taarifa hii. Ushahidi tunao kua ulikua safarini kwahiyo wajipange na siyo kuchafua jeshi la polisi. Akaniruhusu kuondoka. Nilirudi nyumbani huku kichwa kikiwa kimejaa mawazo. Njiani nilikua naongea peke yangu na kuona ni jinamizi gani limeniandamaa. Kwanini nashindwa kummaliza huyu Zabroni Makweka. Kwanini anaua kila anayeonekana kumfuatilia nini ujanja wake.?

Wakati nafika nyumbani kabla sijaingia nilihisi kuna utofauti. Nilihisi ndani mwangu si salama. Nikachukua tahadhari nikatoa bastola yangu na kuingia kwa tahadhari sana. Nilipofika sebuleni nilikuta TV imewashwa. Nikaingia chumbani huko ndo ilikua matatizo. Kwanza niliona mke wangu ametoka povu jingi mdomoni. Pia nilimwona mwanangu wa kumzaa Ametapakaa damu na kichwa kimekatwa. Nilipigwa na butwaa. Nikapepesa macho yule mtoto wa bosi sikumwona. Ghafla________________________
___________________________________________________________________________________________________________________Kutana na mwl Yuu sehemu ya 7, Kwa chochote na kwa simulizi kali kama hizi chek fb kwa jina Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, au Watsap,0755683295, Email, yusuphngahala@gmail.com. Instagram@mwalim_yuu. Chaoooo!!!!!
Previous
Next Post »