MTUNZI-MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA
Sim no 0755683295/Watsap. Facebook.com/Mwalim Yusuph Abel Ng'ahala. instagram@mwalim_yuu.
SEHEMU YA PILI.
Tulipoishia. Nikajisemea moyoni kama ni hivyo nimekwisha. Kisha nikamwambia eenh sema ilo tatizo langu. Akanikazia macho kisha akasema._____endelea..... Tatizo ni kwamba unatuuliza tuu sisi je wewe umefikia wapi mkuu? Roho yangu ikatulia kiasi kisha nikashusha pumzi na kumwambia mimi pia nimefuatilia sana. Nilikusanya pia silaha zilizokutwa siku ya tukio na maganda ya risasi ninavyo hapa. Lakini pia kuna mtu nina taarifa zaka ila haziko sawa nipeni mda nifuatilie kidogo kisha nitaleta taarifa yangu kamili.
Ok, sawa mkuu tumekuelewa alijibu afande peris. Nikawaomba vile vitu walivyovipata wakati wa kupeleleza. Kisha nikawaruhusu waendelee na kazi.Nilimfuata mkuu na kumpa taarifa ile kisha akasema endeleni mwanzo mzuri. Basi Nikawa naumiza kichwa juu ya ile sura yangu kuonekana nimevaa sare za JWTZ, na pianiko kwenye ujambazi. Nikasema haiwezekani lazima nipate ufumbuzi wa swala hili. Wakati natafakari hayo nakumbuka ilikua ni mda wa jioni kama saa kumi hivi. Ndipo tukaitwa kwa ghafla na kuambiwa ya kua kuna majambazi wamevamia sheli moja ya mafuta pale Dar es salaam maeneo ya Ubungo. Tayari kuna vikosi kadhaa vilipelekwa kutoka vituo mbalimbali lakini vilionekana kuzidiwa nguvu. Hivyo tukahitajika kwenda kuongeza nguvu.
Kama ilivyo ada nikapanga vikosi vyangu tayari kwa kuwakabili wahalifu. Tulifika eneo la tukio na kukuta baadhi ya askari wameuawa kikatili sana. Tuliimarisha mashambulizi haswaa mpaka tukafanikiwa kuwaua majambazi wawili. Kwa bahati mbaya wengine wakafanikiwa kutoroka na pesa za ile sheli. Basi tukaichukua miili ya askari wenzetu na ile ya majambazi kwaajili ya shughuli zingine za kiusalama.
Baada ya kufika kituoni ikafanyika kikao cha dharura. Wakuu wa vituo vyote vya kandaa maalumu ya Dar es salaam na baadhi ya maafisa upelelezi kama mimi walikuwepo. Nakumbuka tuliamrishwa na kupewa siku tatu tuwe tumewatia nguvuni majambazi wale waliokimbia. Na zaidi jambazi yeyote la sivyo tunaachishwa kazi. Alisikika mkuu mmoja akisema nchi ina maafisa upelelezi wanashindwa kukamata wahalifu.
Mishahara wanapokea huu ni ujinga. Mwingine akadakia Maafisa upelelezi wote mliopo hapa ili kuokoa kazi tunawataka majambazi hapa ndani ya siku tatu. Kikao kimeisha. Wakuu wetu wa kazi walionekana kuchukizwa na kukimbia kwa majambazi pale sheli. Basi tulitawanyika kila mtu akianza kazi mara moja. Tukapanga siku ya pili jioni tukutane na vielelezo vya kina. Usiku tufanye "operation" ya kuwakamata kisha asubuhi tuwaridhishe wakuu wetu wa kazi. Na zaidi tuwe tumetimiza majukumu yetu.
Basi mimi na wenzangu yaani Afande Peris na Juma. Tulienda pale sheli kuanza kuchukua maelezo. Kuna mhindi mmoja akasema kuna jambazi mmoja anamfamu ni mfanyakazi wa kampuni fulani ya ulinzi pale jijini akatupa anuani ya kufika hapo. Tulienda hadi hapo kisha wote tukashuka na kufunga vizuri gari tukaingia pale kwani hadi picha tulipewa. Kisha tukamwamuru mkuu wao aitishe gwaride ya utambuzi. Basi baada ya askari wake kukusanyika tukakagua na hatukuona mtu.
Kwa kua wengine walikua kazini na hivyo akasema turudi jioni kwa utambuzi mwingine. Tuliondoka tukaingia kwenye gari. Lakini mimi nilipokaa nikahisi nimekalia kitu. Nikainuka na kufunua "seat cover" Mungu wangu nililuta kuna bomu limetegwa. Afande kuna bomu humu tutokeee!!! Niliwambia wenzangu nao wakatoka haraka. Uzuri ni kwamba Afande Juma alikua mtaalamu wa kutegua mabomu akaingia na kuliangalia kisha akalitegua. Ilikua mshituko akaniuliza kama gari niliifunga nikamjibu ndio lilifungwa. Hakuna kioo kilichovunjwa ilikua mshituko kidogo. Baada ya kuanza safari nakumbuka tulikua katika foleni ndipo mtu mmoja akiwa kwenye pikipiki aina ya Honda akaja na kusimama karibu yangu.
Alikua kavalia helment hivyo sikuiona sura kisha akasema mambo nikamjibu safi. Akanirushia bahasha na kuondoka na pikipiki kwa kasi sana. Nilishuka na kujaribu kumfukuzia akawa tayari kaishia zake. Nikarudi ndani na kuifungua bahasha ile na kukutana na ujumbe mzito. Ulikua ukisomeka hivi. "AFANDE YUU NAJUA UNASHANGAA MIMI NI NANI ILA NAKUONYA KAA MBALI NA MIMI, MIMI NDIYE NILIYEWEKA BOMU KWENYE GARI NILIJUA HAMTAKUFA KWASABABU JUMA NI MTAALAMU. ONYO ACHA KUNIPELELEZA UOKOE UHAI WAKO."
Nilijiona ni mjinga niliyeshindwa kumkamata adui mbele ya macho yangu. Nikiwa naduwaa mara foleni ikaanza kusogea. Nikampa Juma barua akaisoma kisha akasema. Hawa watu inaonekana ni hatari sana ni vyema kuwa makini sana. Basi tuliongea mambo mengi na wenzangu mpaka tulipofika kituoni. Baada tuu ya kufika nikashangaa naitwa ofisini.
Niliwahi kwa mkuu nikafika nikapiga saluti kisha nikamsikiliza. Akasema afande kuna tatizo hapa. Kuna ushahidi umeletwa ni mkanda wa video unaonyesha jinsi majambazi walivyokua wakiiba na kuua katika ile sheli. Kumbe ile sheli ilikua na "Cctv kamera" Sasa shida iko hapa katika mkanda ule unaonekana wewe ukiwaua watu na kuwashambulia askari wenzio. Hivi ninavyoongea maafisa upelelezi mkoa wa Dar wanakuja hapa kwaajili ya kuongea na wewe. Nilipigwa na butwaa nikahisi dunia inanigeukia. Mimi niliongoza vikosi kukabiliana na majambazi ni vipi nahusika? Nikameza mate funda moja. Woga ukaniingia kisha nikamgeukia mkuu na kumwambia.
Mkuu wewe ni shahidi mimi ndiye niliongoza operation baada ya wenzetu kuzidiwa. Mimi ni Afande mwaminifu unanijua tangu zamani. Nahusikaje kwenye uhalifu? Mkuu akajibu kwa mkato Video inaonyesha hivyo. Nikajikuta naishiwa nguvu. Nikaanza kuona kama nafanyiwa mchezo. Mara nikasikia tunaitwa nje Maafisa upepelelezi tayari wamefika kujadili swala langu ikiwemo mimi kuhojiwa. Tulisimama na kuelekea ukumbi wa mikutano ya dharura. Huko wakati tunaingia nilikuta maafande wenzangu wakiniangalia macho ya husda. Nikajisemea moyoni Mungu we unajua ukweli wa yote. Mara nikasikia sauti ya kamanda wa usalama kanda maalumu ya Dar es salaam. Aliongea huku akinitaka nikae katikati nohojiwe juu ya tukio lile. Huku afisa mzima nikionekana naua watu. Baada ya kukaa maswali yalianza hivi__________________________
EmoticonEmoticon