Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima.
Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote.
Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano.
Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio.
Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.
Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.
Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.
Wakati
taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya jamii kuwa nyumba ya
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imezingirwa na
polisi, habari kamili ni kwamba zoezi la kumkamata askofu huyo
lilishindikana baada ya kugoma kufungua geti lake.
Polisi
hao waliokuwa na silaha walifika nyumbani kwa askofu huyo maeneo ya
Salasala jijini Dar wakiwa kwenye magari zaidi ya manne ambapo walipiga
kambi katika eneo hilo kwa saa sita huku njia hiyo ikiwa imefungwa kwa
saa kadhaa kabla ya waandishi wa habari na baadhi ya waumini wa askofu
huyo kuruhusiwa kupita.
Hata
hivyo baada ya polisi hao kuzungumza na mawakili wa Gwajima na viongozi
kadhaa wa kanisa hilo, waliamua kuondoka huku wakitoa amri kiongozi
huyo afike kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi ambapo
alifika na baadaye kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu ambapo
alisomewa mashitaka mawili ya kutoa lugha ya matusi na kushindwa kutunza silaha.
Askofu huyo ameachiwa kwa dhamana na kesi yake itaendelea Mei 4 mwaka huu.
EmoticonEmoticon