Wavamizi
walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo
kabla ya wavamizi kuingia wakiwa wamejihami kwa bundukiWatu 17
wameripotiwa kuuawa na wengine 20 kujeruhiwa vibaya wakati wanamgambo wa
Kiislamu wa Al Shaabab waliposhambulia majengo ya wizara ya elimu mjini
Mogadishu,Somalia.
Mwandishi wa BBC Mohammed Moalimu,amesema kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo.
Kulingana
na msemaji wa idara ya usalama wa ndani Mohammed Yusuf watu 8 waliuawa
na wavamizi hao huku wanajeshi wawili wakipoteza maisha yao.
Askari mmoja ni wa muungano wa majeshi ya umoja wa Afrika.
Msemaji
huyo anasema kuwa wavamizi hao walikuwa ni 7 wawili waliojilipua langoni
huku wengine watano wakikabiliwa na maafisa wa usalama.
Walioshuhudia
wanasema wavamizi hao walitumia bomu lililotegwa ndani ya gari kabla ya
wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo wakiwa wamejihami kwa bunduki za
rashasha.
Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi la wapiganaji wa Al Shabaab Sheikh Abdiasis Abu Musab, amethibitisha kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi hilo na kuwa ''wapiganaji wetu wamekwisha ingia ndani ya jengo hilo lenye wizara ya elimu''
Mapigano
yanaendelea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya majeshi ya serikali
na wapiganaji hao kulingana na mwakilishi wa polisi.
Wapiganaji wa Al shabaab wametekeleza mashambulizi kama haya katika siku za hivi punde.
Mwezi
uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini
Mogadishu uvamizi huo ulikamilika siku mbili zilizofwatia .
Waandishi
wa habari walioshuhudia matukio kabla ya uvamizi huo wanadai kuwa
kulikuwa na milipuko miwili mikubwa kabla ya milio ya risasi kuanza
kusikika kutoka jengo hilo.
hakuna kundi lililothibitisha kutekeleza shambulizi hilo lakini Al shabaan imekuwa ikitumia mbinu kama zilizotumika leo .
Kundi hilo la waislamu linapinga serikali iliyoko sasa ambayo inaungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika.
EmoticonEmoticon