Mwili wa AK47 ukitolewa katika mochwari ya Hospitali ya Nsambya.
WAKATI
wapenzi wa muziki nchini Uganda wakiwa bado wamegubikwa na simanzi kwa
kuondokewa na mwanamuziki wa miondoko ya dancehall, Emmanuel Mayanja
maarufu kwa jina la AK47, taarifa mpya zimeibuka kuwa kuna uwezekano
kuwa alipigwa kabla ya kifo chake.
Jose Chameleon (katikati) akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mdogo wake.
AK47 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali baada ya kuanguka akiwa bafuni.
Taarifa
hizo zinadai kuwa atakuwa alipigwa katika baa aliyokuwemo iitwayo
Dejavu, iliyopo eneo la Kabalagala kabla ya kupelekwa Hospitali ya
Nsambya, Kampala ambapo mauti yalimkuta.
Pallaso (mwenye tisheti ya bluu) ambaye naye ni kaka wa marehemu akifarijiwa na mwanamuziki Bebe Cool.
Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kabalagala, Nusulah Kemigisha ameeleza
kuwa anahisi kuna mchezo mchafu umechezwa baada ya kukuta mwili wa
marehemu ukiwa na majeraha sehemu za kifua na kuamua kufunga baa hiyo
ili kuruhusu uchunguzi.
Marehemu AK47 enzi za uhai wake.
Imeelezwa
kuwa AK47, ambaye ni mdogo wa mwanamuziki nguli wa Uganda, Jose
Chameleon (Joseph Mayanja), alipigwa na kuamua kwenda bafuni kunawa
kabla ya kudaiwa kuteleza na kuanguka.
EmoticonEmoticon