Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilayani Momba Mkoani Mbeya kimelaani tukio lililotendeka jana la baadhi ya wananchi kupigwa na kujeruhiwa na Jeshi la Polisi akiwemo Diwani wa kata ya Tunduma Frenk Mwakajoka.
Akizungumza na kituo hiki katika ofisi ya Mbunge wa Momba katibu wa mbunge Maarifa Mwashitete amesema kitendo kilichofanywa jana na jeshi la polisi si la kiungwana na halifai kuvumilika katika jamii kwani suala hilo si la kisiasa bali ni la kijamii.
Amesema tukio lililotokea jana jeshi la polisi lilidai kuwa walikuwa wanazuia mikutano au mihadhara isiyokuwa halali iliyokuwa ikiendelea katika mtaa wa Sogea jambo ambalo si la kweli kwani wananchi walikuwa katika maendeleo ya ujenzi wa Zahanati katika eneo la makaburini ili kusogeza huduma hiyo karibu.
Aidha Mwashitete wahisihi jeshi la polisi kutumia Diplomasia kwa kuweza kutatua matatizo katika jamii na si kutumia mabomu ya machozi,kwani kwa kufanya hivyo wanawaadhiri watu wasiokuwa na hatia.

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng