TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 01.12.2014.
MTU MMOJA ANAYEDAIWA
KUWA NI KIBAKA AMEUAWA KWA KUPINGWA NA KUNDI LA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI.
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EMANUEL EDWARD
(29) MKAZI WA ILOMBA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA
MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA
SILAHA ZA JADI FIMBO, RUNGU NA MAWE KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI.
INADAIWA KUWA
AWALI MNAMO TAREHE 30.11.2014 MAJIRA
YA ALFAJIRI HUKO ENEO LA BLOCK – T,
KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA MAREHEMU ALIKUTWA AKIWA
KATIKA HARAKATI ZA KUIBA NYUMBANI KWA ERICK
ANYASWILE (53) MFANYABIASHARA, MKAZI WA BLOCK –T AMBAYE ALIPIGA KELELE ZA
KUOMBA MSAADA NA WANANCHI HAO KUJITOKEZA NA KISHA KUMSHAMBULIA MAREHEMU.
INADAIWA KUWA
MAREHEMU ALIVIZIA WAKATI GETI LA NYUMBA HIYO LIMEFUNGULIWA NA KUINGIA NDANI KWA
NIA YA KUFANYA UHALIFU HUO NA NDIPO MMILIKI WA NYUMBA HIYO ALIMUONA NA KISHA
KUOMBA MSAADA. AIDHA INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA NI MWIZI [KIBAKA] MZOEFU
ALIYESHIRIKI MATUKIO MENGI YA KIHALIFU.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI
KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA
WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. AIDHA ANATOA
WITO KWA JAMII KUTAFUTA KIPATO CHA NJIA ZILIZO HALALI ILI KUEPUKA MATATIZO
YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon