Watanzania
waendelea kufaidika kutoka kwa hospitali ya Apollo iliyoko nchini
India. Hii ni kufuatia hosiptali hiyo kufanikiwa kuwatenganisha mapacha
wa kike Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na
tumboni kutoka nchini Tanzania katika upasuaji uliofanyika tarehe 17
Novemba 2014 nchini India. Mapacha waliounganika kwa mtindo huu
hujulikana kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji
uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.
Mapacha Abriana na Adriana awali ya
upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya kifua na tumbo, hali
kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo na maini
yaliyounganika. Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa kwa madaktari
ulikuwa kufanya utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi ambayo
waliweza kukabiliana nayo ipasavyo kutokana na madaktari waliokuwepo
wenye wataalum wa kiufundi na matibabu.
Upasuaji huo ulifanywa na jopo la
watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbali mbali za tiba ya afya ya
kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa masaa 11. Watalaamu
walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyo kuwa vimeungana lakini mapacha
hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo kusaidia zoezi zima la
uponyaji baada ya upasuaji.
Hali kadhalika, hatua nyingine ya muhimu
katika upasuaji huo ilikuwa kurudisha viungi husika katika mahala pake
baada ya kuvitenganisha. Akizungumzia kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar
Plastic & Reconstructive Surgeon anasema, “Baada ya upasuaji, moyo
wa moja ya mapacha ulitakiwa kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko
na uharibifu pamoja na maini yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo
mawili ya wataalum kwa masaa nne kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na
utumbo katika mahala pake.”
Upasuaji huu wa mafanikio wa mapacha
waliounganika kutoka ncini Tanzania sio wa kwanza kufanywa na hospitali
ya Apollo. Mwishoni mwa mwaka 2013 mapacha wengine wakiume waliokuwa
wameungana na kujulikana na wataalamu kama Pygopagus, Ericana &
Eluidi kutoka Tanzania walifanikiwa kutenganishwa na wataalamu wa
hospitali hiyo. Matukio amabayo yamepandisha chati na kuipa hadhi ya juu
hospitali ya Apollo iliyoko nchini India na nchi ya India kwa ujumla
kama kiongozi katika sekta ya afya na mfano wa kuigwa na nchi nyingine
ikiwemo Tanzania. Hospitali hiyo ina mahusiano mazuri na nchi ya
Tanzania ikitembelewa idadi kubwa ya wagonjwa kutoka Tanzania kutokana
na ukosefu wa huduma muhimu na za kisasa nchini.
Wapacha walioungana hutambuliwa na
kupewa majina kutokana na jinsi muungano huo unapokuwa katika viungo
mbali mbali vya mwili. Ikiwa aina ya mapacha waliounganika wa Thoraco
Omphalopagus ndio inayoongoza kuripotiwa kwa asilimia 28% zaidi ya aina
nyingine zote zinazotambulika matukio mengi yakitokea zaidi
Kusini-Magharibi mwa bara la Asia, Africa and Brazili. Katika aina hii
mapacha wanakuwa wameunganika kuaznia kifuani mpaka chini ya kifua
kwenda kwenye tumbo na hutumia baadhi ya sehemu ya moyo, ini na baadhi
ya sehemu viungo vya mmeng’enyo wa chakula(i).
Kulingana na hospitali ya Apollo kesi
zinazohusu mapacha waliounganika huwa ni nadra mathalan moja kati ya
uzao 200,000 huonekana. Lakini, asilimia 60 ya hao hufariki wakati
asilimia 35 hufariki katika kipindi kifupi baada ya kuzaliwa kutokana na
sababu mbali mbali (ii).
Akizungumzia upasuaji huo uliokuwa na
mafanikio, Dkt. Prathap C Reddy, Mwenyekiti na Muanzilishi wa Hospitali
za Apollo anasema, “Nikitazama katika mwaka huu wa 2014 naona maisha ya
watu tuliweza kuyagusa kwa namna njema. Mbali na maumivu wanayopata
watoto yatokanayo na ugonjwa, wazazi pia hupitia mshituko na mahangaiko
makubwa. Nchi nyingi za bara la Afrika zinakosa tiba muhimu na mbadala
na hivyo kujikuta wanakuja nchini India kupata huduma hizo muhimu na
kisasa. Inafurahisha na kuleta faraja kuwa katika sikukuu hii ya
Krismasi Jimmy na Carolyn watarudi nyumbani na watoto wao wakiwa ni
binadamu wawili tofauti.”
Tangu mwaka 2007, jozi nane za
mapacha waliounganika katika ini na utumbo kutoka sehemu mbali mbali
nchini India zimeripotiwa kutenganishwa. Aradhana na Stuthi ni jozi
pekee ya mapacha waliwahi kutenganishwa kwa upasuaji wakiwa na mioyo
iliyo katika mvungu (cavity) mmoja hali sawa na mapacha Adrianan na
Abriana. Japo moja ya mapacha wa thoraco opmhalopagus Aradhana kufariki
wiki tatu baadae, Adriana and Abriana na ndio aina hiyo ya mapacha
walioweza kuishi baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa.
Baada ya miezi ya matibabu, mapacha
Adriana na Abriana kutoka Dar-es-Salaam watarejea nyumbani Tanzania
tarehe 18 Disemba na kufika mjini Dar es Saaam asubuhi ya tarehe 19
Disemba. Katika kipindi hiki cha sikukuu itakuwa shangwe kwa wazazi
Jimmy na Carolyn wanaporudi nyumbani kutoka nchini India wakiwa na
watoto wao wawili waliotenganishwa.
EmoticonEmoticon