TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 13.11.2014.
Ø MTOTO
MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA KUGONGWA NA PIKIPIKI WILAYA YA KYELA.
Ø WANAFUNZI
WATATU WA KIKE WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WILAYA YA
ILEJE.
TUKIO LA KWANZA.
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA RUNGU KICHWANI WILAYA YA CHUNYA.
MTU
MMOJA GASPER
VISENTI [38], MKAZI WA KIJIJI CHA KALANGALI
ALIKUTWA AMEUAWA PORINI BAADA YA KUPIGWA RUNGU KICHWANI NA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MOJA LA
CLEMENT
SIMKOKO @ YOHANA, MKAZI WA [W] MBOZI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 12.11.2014 MAJIRA YA SAA
16:15HRS KATIKA KITONGOJI CHA IVUMWE,
KIJIJI CHA KALANGALI, KATA YA MTANILA, TARAFA
YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA. MWILI WA
MAREHEMU ULIKUTWA UKITOKA DAMU NYINGI PUANI NA MASIKIONI. CHANZO CHA TUKIO HILI NI KULIPIZA KISASI BAADA
YA MAREHEMU KUMDHURUMU MTUHUMIWA PESA UJIRA WAKE BAADA YA KUMLIMIA SHAMBA LA
TUMBAKU. HATA HIVYO MTUHUMIWA HUYO ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI AN AENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA PIA KUEPUKA MATATIZO YANAYOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZIWEZE KUCHUKULIWA MARA
MOJA.
TUKIO
LA PILI.
MTOTO MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA
AJALI YA KUGONGWA NA PIKIPIKI WILAYA YA KYELA.
MTOTO
MMOJA AITWAE MICHAEL MICHAEL [4], MKAZI WA NDANDALO ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO
BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI T.207 CUV AINA YA SUNLG ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA
MOSE ANDREW [22],MKAZI WA NDANDALO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 12.11.2014 MAJIRA YA SAA
12:30HRS KATIKA KIJIJI CHA NDANDALO,
KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA
YA KYELA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO
KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOEPUKIKA.
TUKIO
LA TATU.
WANAFUNZI WATATU WA KIKE WAFARIKI
DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WILAYA YA ILEJE.
WANAFUNZI WATATU WA KIKE WANAOSOMA SHULE YA MSINGI ILOMBA AMBAO NI 1. SEVELINA MWILE [11], MKAZI WA
KITONGOJI CHA ITALE 2. GRACE PATSON [10], MKAZI WA KITONGOJI CHA ITALE
NA 3. AGEY SEME [10], MKAZI
WA KITONGOJI CHA ILOMBA[W] MBEYA VIJIJINI
WOTE WANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULENI HAPO WALIFARIKI DUNIA BAADA YA
KUFUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WAKATI WAKICHIMBA UDONGO NDANI YA SHIMO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 12.11.2014
MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA
KITONGOJI CHA ILOMBA, KATA YA ITALE,TARAFA YA BUNDALI WILAYA YA ILEJE MPAKANI
NA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI,MKOA WA MBEYA. AWALI KABLA YA KUKUTWA NA MAUTI WAHANGA HAO WALICHUKULIWA SHULENI NA ISAMBI MWASENGA [57], MWALIMU MKUU
MSAIDIZI WA S/MSINGI ILOMBA KWENDA KUMFANYIA
KAZI BINAFSI YA KUCHIMBA UDONGO NA KUMPELEKEA NYUMBANI KWAKE. MIILI YA MAREHEMU
IMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA
AMEKAMATWA NA YUPO MAHABUSU KWA AJILI YA USALAMA WAKE WAKATI UPELELEZI WA
SHAURI HILI UKIENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUWATUMIKISHA KAZI WATOTO WENYE UMRI MDOGO KATIKA
MAENEO/MAZINGIRA HATARISHI YATAKAYOWEZA KUSABABISHA MAAFA NA KUFANYA VITENDO
VYA NAMNA HIYO NI KWENDA KINYUME CHA SHERIA.
Imesainiwa;
[ AHMED
Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon