Kijana
Sande Mrema Mwenye tatizo la uzito wa kilo 250 na umri wa maiaka 25
ameshindwa kusafiri kwenda nchini india katika matibabu yake baada ya
kushushwa mara kadhaa kwenye ndege za kimataifa anazotakiwa kusafiria
licha ya ndugu zake kulipa Gharama zote za usafiri wake.Akizungumza kwa
Masikitiko eneo la karakana katika moja ya Hoteli anapoishi kwa sasa
wakati akisubiri miujiza ya kupatikana kwa Ndege Bwana Sande Mrema
aliyehitaji waandishi kumfunika uso wakati wa mahojiano amesema
anateseka sana na uzito wake unazidi kuongezeka siku hadi siku lakini
hajafanikiwa kusafiri.
Dada wa
mgonjwa huyo anaeleza namna ambavyo wameteseka kumuhudumia ndugu yao
mapaka sasa na Kuomba serikali kuingilia kati kufanyanikisha safari ya
ndugu yao kwani ameshawasiliana na Daktari wake na malipo wameshafanya
ila tatizo ni kupatikana kwa nafasi katika Ndege.
Licha ya
ITV kujaribu kutafuta wahusika wa Ndege hizo na kushindikana kwa
leo,mama mdogo wa kijana huyu anaelezea ndege walizolipia na
kushindikana hivyo kuomba waziri wa afya na ustawi wa jamii,waziri wa
uchukuzi na viongozi wengine kuwasaidia ili nafasi ya kusafiri
kupatikana.
EmoticonEmoticon