Wanafunzi wa bweni ambao ni walemavu wa ngozi na wasioona
wanaohifadhiwa na serikali katika shule ya msingi pongwe jijini tanga
wameiomba Serikali kwa kushirikiana na wasamaria wema kuwajengea uzio
shuleni hapo kufuatia kutembea umbali wa mita 100 wakati wanapokwenda
kujisaida nyakati za usiku hatua ambayo inahatarisha usalama wao.
Wakizungumza shuleni hapo wakati wasamaria wema walipokwenda
kuwasaidia wanafunzi walemavu wa ngozi na vipofu vifaa mbali mbali
ikiwemo vya kusaidia walemavu wenye uono hafifu,wanafunzi hao wamesema
wameanza kuingiwa na hofu ya kuuawa kufuatia nyakati za usiku na
kulazimika kwenda nje ya mabweni yao kujisaidia ambayo yapo umbali wa
mita 100 kutoka eneo wanalolala ambako hakuna uzio.
Kwa upande wake mwalimu wa mlemavu asiyeona anayefundisha shule hiyo
maalum Bwana Jumaa Mwachalika ameiomba serikali kuharakisha zoezi la
kuwaingiza katika teknlojia ya tehama kwenye masomo yao kwa sababu
wangepata vitendea kazi ikiwemo kompyuta maalum kwa watu wasioona
vingeweza kuwasaidia kufanya vyema kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wasamaria wema waliojitokeza kuwasaidia
walemavu hao vifaa mbali mbali ikiwemo mashine za kuwaongezea uwezo
walemavu wenye uono hafifu,wameiomba jamii kujitokeza kusaidia walemavu
hao kutoka mikoa mbali mbali nchini ambao wamehifadhiwa katika shule
hiyo ya bweni kutokana na sababu za kiusalama kufuatia wenzao walemavu
wa ngozi kuuawa kikatili na baadhi ya watu.
EmoticonEmoticon