TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 08.10.2014.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA
BAADA YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA RAIA
NA MKAZI WA WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30 AMEFARIKI DUNIA
WAKATI AKIWA ANAPATIWA MATIBABU BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.397 AQT AINA YA ISUZU LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE NOEL
MAHENGE KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.505 BYG/T.843 CUG AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE GODFREY PHILIMON (37) MKAZI WA TUKUYU
WILAYA YA RUNGWE.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 07.10.2014
MAJIRA YA SAA 09:45 ASUBUHI HUKO
CHAPWA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.
AIDHA, KATIKA
AJALI HIYO WATU WAWILI WALIJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI
TUNDUMA AMBAO NI 1. SHABANI KIPANDE
(22) MKAZI WA UYOLE NA 2. MUDDY MSELEMU
(25). CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.397 AQT AINA YA ISUZU. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA
JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA SERIKALI VWAWA – MBOZI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA,
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEKIMBIA
KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AITWAYE SEYIM LATABO (45) KWA KOSA LA KUINGIA
NCHINI BILA KIBALI.
MHAMIAJI HUYO
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.10.2014 MAJIRA YA SAA 07:50 ASUBUHI HUKO KATIKA STENDI YA MABASI – TUKUYU, KATA YA
KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA
AMESHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAGENI
KUFUATA TARATIBU ZA KUINGIA NCHINI ILI KUEPUKA MATATIZO NA MADHARA YANAYOWEZA
TOKEA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon