Meneja
wa Masoko na mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania,
Ngula Cheyo (katikati) akiongea na wandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa utambulisho wa huduma ya Mikopo ya bidhaa.(Picha zote na
Andrew Chale).
Na Andrew Chale
Taasisi
ya kifedha ya Bayport Tanzania mapema leo Oktoba 15, 2014 imezindua
huduma mpya ijulikanayo kama Mikopo ya bidhaa ikiwa na lengo la
kurahisisha utendaji kazi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wote wa
kampuni zilizoidhinishwa na Bayport.
Uzinduzi
huo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Bayport, maeneo ya Moroco
jijini Dar es Salaam mbele ya wandishi wa vyombo mbalimbali vya habari
umeonyesha matumaini mapya ya watanzania wanaosumbukia usafiri katika
vituo vyao vya kazi, hususani maeneo ya mikoani ambako mara kadhaa
kumesikika malalamiko ya maisha magumu kwa watumishi wa umma.
Akizungumza
juu ya tukio hilo, Meneja Bishara wa taasisi hiyo Thabit Mndeme alisema
kwamba ni wakati wa kukuza uchumi wa nchi kuhakikisha kuwa watu
wanafanya kazi kwa bidii na shauku.
Meneja
wa Masoko na mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania,
Ngula Cheyo (wa kwanza kushoto), akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja
masoko wa Fair Deal Auto (pvt) Limited, wasambazaji wa pikipiki aina ya
Boxer na Bajaji, Saimon Paul pamoja na Meneja Bishara wa Bayport,
Thabit Mndeme (kulia), wakati wa utambulisho wa kuzindua huduma hiyo ya
Mikopo ya bidhaa.
Alisema
wapo watumishi ambao wanaishi kwa tabu kutokana na changamoto ya
usafiri na mahitaji mengine ya kijamii ,hivyo kutokana na huduma hiyo
mpya ya kukopeshwa pikipiki ,boda boda itasaidia kwa kiasi chake.
Pia
alisema Bayport imekaa kuangalia namna gani watanzania wataendelea
kufanya kazi kwa moyo na kukuza uchumi ambao uko sambamba na
kuwakopesha fedha kama wanavyofanya kwa sasa na kuamua kuwakopesha tena
na bidhaa za usafiri.
Naye
Meneja wa Masoko na mawasiliano wa taasisi hiyo Ngula Cheyo alisema
kuwa mikopo mipya kwa sasa inapatikana kwa masaa 24, huku ikipatikana
pia kwa mikoa na wilaya zote kwenye ofisi za Bayport zaidi ya 80,
nchini.
Bayport
ni Taasisi ya kifedha isiyo ya kibenki inayoongoza katita utowaji wa
mikopo barani Afrika na Amerika ya kusini imeanzishwa mwaka 2001, na
umiliki wake ukiwa Mauritius.
Meneja
wa Masoko na mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania,
Ngula Cheyo (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na Meneja masoko wa Toyo,
Drima Makachwa (katikati) pamoja na Meneja Bishara wa Bayport, Thabit
Mndeme (kulia), kwenye uzinduzi huo.
EmoticonEmoticon