· WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.







TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 09.09.2014.


·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI WA NG’OMBE.

·         WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.

·         MTOTO WA MIAKA MIWILI (02) AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA LEVIS MLENGA (43) MKAZI WA LUFITA NCHINI MALAWI ALIFARIKI DUNIA AKIWA AMEFUNGIWA KATIKA CHUMBA KIMOJA KATIKA OFISI YA KATA BAADA YA KUPIGWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI WA NG’OMBE WAWILI MALI YA EMMANUEL KILEMBE, MKAZI WA KIJIJI CHA ILONDO.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 06.09.2014 HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MALANGALI, TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA ILEJE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKAMATWA NA ASKARI POLISI WA NCHINI MALAWI NA ALIPOJARIBU KUTOROKA NDIPO WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMKIMBIZA NA WALIPOMKAMATA WALIANZA KUMSHAMBULIA NA KUMSABABISHIA MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWANI HALI ILIYOPELEKEA KUTOKWA DAMU PUANI NA MDOMONI.

AIDHA, WATU WATATU WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. EMMANUEL KILEMBE 2. ITISON NDIMBWA WOTE WAKAZI WA ILONDO NA 3. FURAHA KIBONA, KAIMU MTENDAJI KATA YA MALANGALI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA – ITUMBA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.



KATIKA TUKIO LA PILI:

WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. MORTINA (30) 2. EDINA JASON (22). 3. PAULO MWANYALILA, PADRI KANISA LA ROMANI CATHOLIC KYELA NA MWANAMKE MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE MARA MOJA WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA MAGARI MAWILI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.241 BKZ AINA YA TOYOTA COASTER IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE KUGONGANA NA GARI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 08.09.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO MAENEO YA GARIJEMBE, KATA YA UTENGULE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WATATU WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. SAMWEL ASANGA (34) 2. MAWAZO GASPER NA 3. MTOTO WA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 02 – 03 AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE.

CHANZO CHA AJALI HIYO BADO KINACHUNGUZWA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO. MADEREVA WA MAGARI YOTE MAWILI WALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI HIYO, JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA.







KATIKA TUKIO LA TATU:

MTOTO WA MIAKA MIWILI (02) ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA GROLIA LEVOKATUS MKAZI WA ITEWE AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 08.09.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO ITEWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/IRINGA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. PIA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU NA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUVUTA MAENEO YENYE VIVUKO. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA [MADEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »