RB namba WH/RB/6335/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo Hill, Tegeta jijini Dar, imemtia mbaroni mtangazaji maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu ‘Lady Hanifa’ na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Aneth kwa madai ya kutaka kumuua mhudumu wa baa aliyetambulika kwa jina la Aika Andrew (32).
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba sakata hilo la kusikitisha lilijiri wiki iliyopita kwenye baa maarufu ya Shayo iliyopo Tegeta, Dar.
Maelezo yaliyoandikishwa na Aika polisi yalidai kwamba Lady Hanifa alifika kwenye baa hiyo ambayo ndani yake anamiliki jiko la chakula na kuelezwa kwamba, siku moja kabla ya tukio hilo alikuwa na deni na alipofika tu, Aika alimkumbushia ndipo balaa lilipoanza.
Mhudumu wa baa anayetambulika kwa jina la Aika Andrew (32) aliyenusurika kuuawa na mtangazaji maarufu Bongo, 'Lady Hanifa' .
Kwa mujibu wa mashuhuda, katika tukio hilo lililojiri mishale ya saa 11:00 jioni, Hanifa alipofika aliingia moja kwa moja jikoni kuangalia biashara yake kisha akarudi kukaa sehemu ya baa.
Ilisemekana kwamba Aika alimfuata na kumwambia kuwa jana yake alikuwa akidaiwa bia moja tu ya baridi aliyokuwa amekopa, kitendo kilichompandisha hasira na kuona kama amefedheheshwa kudaiwa mbele za watu.
Ilidaiwa kwamba alimwita mfanyakazi wake, Aneth ili ampatie fedha aliyokuwa akidai Aika lakini muda huohuo Lady Hanifa akaanza kudai chenji yake kwa mabavu.
Ilidaiwa kwamba kulitokea majibizano makubwa ndipo mtangazaji huyo akaanza kumshambulia Aika huku akipewa sapoti na Aneth.
Iliendelea kudaiwa kwamba katika purukushani hizo, Aneth aliyekuwa ameshika kisu alimchoma nacho Aika tumboni, kichwani, mikononi huku Lady Hanifa akimuunguza shingoni kwa kutumia upawa wa chipsi uliokuwa na mafuta ya moto kisha wakakimbia.
Habari zilieleza kwamba baada ya hapo Hanifa na Aneth walikimbilia Kituo cha Wazo Hill kutoa taarifa lakini muda mfupi wasamaria wema walifika katika kituo hicho wakiwa na Aika aliyekuwa ametapakaa damu mwili mzima.
Polisi waliwashikilia Lady Hanifa na Aneth na Aika akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.
CREDITS:GPL
EmoticonEmoticon