TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15.08.2014.
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI JIJINI MBEYA.
WATU WAWILI
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LYDIA LUVANDA (45) MKAZI WA FOREST YA ZAMANI NA 2. FELIX MAHENGE (18)
MKAZI WA FOREST WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA
USAJILI T. 979 BNB AINA YA TOYOTA MARK
II LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA
AITWAYE RICHARD MATIKU (27) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA FOREST.
AJALI HIYO
IMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA
02:00 HUKO KADEGE, KATA YA FOREST, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WATATU [03]
WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. MESS ROGERS
(27) MKAZI WA FOERST 2. AGATHA ANGETILE (32) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA FOREST NA 3. FIBI LULELA (18)
MWANAFUNZI SHULE YA FINERIA ACADEMY NA MKAZI WA FOREST.
CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
NA MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI BADO LIPO
ENEO LA TUKIO.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na kutolewa
na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon