TRAFIKI ANUSURIKA KIFO BADA YA KUGONGWA NA GARI!


#HABARI TRAFIKI AGONGWA NA GARI!

Askari mmoja wa kikosi cha usalama barabara ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, amenusurika kufa baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki ya polisi, ambayo ilikosa mwelekeo na kugongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za usajili T 681 CUX eneo la Bamaga Mikocheni jijini Dar es salaam.


Askari mmoja wa kikosi cha usalama barabara ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja amenusurika kufa baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki ya polisi ambayo ilikosa mwelekeo na kugongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za usajili T 681 CUX eneo la Bamaga Mikocheni jijini Dar es salaam ambapo gari hilo lilikuwa likiandeshwa na mwanamke mmoja huku mashuhuda wa ajali hiyo kila mmoja amekuwa na mtazamo tofauti juu ya matumizi ya barabara nyakati za jioni hadi ajali hiyo ikatokea.

Previous
Next Post »