Ni msimu mwingine wa machungwa, yamejaa tele kila kona. Shilingi 100 tu unapata chungwa. Lakini siyo ajabu kama kuna watu msimu unaisha hawajala hata chungwa moja, wala suala la matunda halipo kabisa katika orodha ya milo yao!
Inawezekana pia hata kwa wale wanaokula, japo kidogo, hula kama kiburudisho tu bila kujua faida zake mwilini. Katika makala ya leo nitakujuza faida 13 unazoweza kuzipata unapokula chungwa, ambalo limesheheni virutubisho kibao.
Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.
1. UKOSEFU WA CHOO
Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.
2.UGONJWA WA MOYO
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!
3. SHINIKIZO LA DAMU
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.
4. UGONJWA WA MAPAFU
Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.
5. MIFUPA NA MENO
Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.
6. AFYA YA NGOZI
‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’.
7. KOLESTRO
Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.
8. UKUAJI WA UBONGO
Chungwa moja lina kiasi cha asilimia 10 ya ‘folic acid’ inayohitajika mwilini kila siku. Madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri.
9. KINGA YA MWILI
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.
10. UGONJWA WA FIGO
Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.
11. VIDONDA VYA TUMBO
Unapokuwa na kiwango cha kutosha cha Vitamin C mwilini, una uhakika na kinga dhidi ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo, na kama tayari unavyo, ulaji wa machungwa utakupa ahueni.
12. UGONJWA WA MAFUA
Kutokana na wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula machungwa mengi kadii uwezavyo ili ujiepushe na mafua.
13. KINGA YA MAGONJWA MENGI
Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu, nimonia na kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili kupata faida hizo.
Leo katika makala haya, natarajia kukujuza faida na umuhimu wa tunda hili ambalo wengi wetu tunalichukulia kirahisi sana na pengine hatujui hasara tunazozipata pale tunapoacha kulila. Kama ilivyo ada ya kona hii, tunasema kwamba jinsi ulivyo kiafya leo ni matokeo ya ulaji wako wa jana na juzi, jinsi utakavyokuwa kiafya kesho na keshokutwa, ni matokeo ya ulaji wako wa leo na kesho.
FAIDA ZA CHUNGWA KIAFYA
Katika utafiti wa hivi karibuni uliofanywa kwenye tunda la chungwa, iligundulika kwamba tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuponya matatizo mbalimbali ya kiafya kwa sababu lina mkusanyiko mkubwa wa virutubisho vya Phytonutrients.
Jamii ya virutubisho hivyo inajumuisha pamoja na citrus flavanones, anthocyanins, hydroxycinnamic acids na polyphenols, ambapo inaelezwa kwamba virutubisho hivyo vinapochanganyika na Vitamin C inayopatikana kwenye chungwa, uwezo wake wa kutoka kinga mwilini huwa mkubwa.
Moja ya faida nyingi za virutubisho hivyo ni pamoja na kushusha kiwango cha shinikizo la damu pamoja na kiwango cha mafuta mabaya mwilini, maarufu kwa jina la Kolestro. Jambo la muhimu kuzingatia sana hapa ni kwamba virutubisho vingi muhimu vinapatikana kwenye maganda na nyama nyeupe ya chungwa na siyo kwenye maji peke yake.
Kwa maana nyingine ili upate vitamini na virutubisho vyote muhimu vinavyopatikana kwenye tunda la chungwa, inashauriwa kulila pamoja na nyama zake, na siyo kukamua maji peke yake. Ingawa wa kufanya hivyo bado una uhakika wa kupata Vitamin C ambayo ndiyo inapatikana kwa wingi kwa kunywa juisi yake tu.
UNAUJUA UMUHIMU WA VITAMIN C ?
Bila shaka utakuwa unaelewa tangu zamani kwamba chungwa ni chanzo kikubwa cha Vitamni C, kwani chungwa moja lina uwezo wa kutoa hadi asilimia 116 ya kiwango kinachotakiwa kwa siku, lakini pamoja na kujua hilo, unafahamu Vitamini C na machungwa kwa ujumla ni muhimu kiasi gani katika afya yako?
Kwanza kabisa Vitamini C hutoa kinga ya mwili kupambana na maradhi kama vile mafua, kikohozi na hata kifua kikuu na vile vile huondoa vijidudu nyemelezi (free radicals) mwilini na kuzipa seli kinga madhubuti ya kutoharibika, nje na ndani.
Inaelezwa kwamba hatari kubwa ya kwanza seli inapokuwa haina kinga dhidi ya vijidudu nyemelezi, ni kupatwa na saratani, hasa ya utumbo. Lakini ukiwa na Vitamni C ya kutosha mwilini, unakuwa umejitengenezea kinga madhubuti dhidi ya saratani hiyo.
Aidha seli zinapokuwa zimedhurika kwa kukosa kinga, mwili mzima huwaka moto kwa maumivu, hasa wakati mwili unapokuwa ukijaribu kuondoa seli zilizodhurika. Hivyo inaelezwa kwamba Vitamin C, ambayo ndiyo huzuia vijidudu nyemelezi vinavyosababisha maumivu ya mwili kuongozeka, hutoa nafuu zaidi kwa magonjwa hayo na mengine kama pumu na viungo.
Vilevile vijidudu nyemelezi (free radicals) ndivyo vinavyosababisha kuganda kwa kolestro mwilini ambapo inapofikia hali hiyo husababisha kuziba kwa mishipa ya damu na mwisho huleta mshituko wa moyo au kiharusi. Lakini kwa mwili kuwa na Vitamin C ya kutosha, hali hiyo haiwezi kutokea kwani Vitamin hii ina uwezo wa kudhoofisha vijidudu hivyo visilete uharibifu.
GLASI MOJA YA JUISI NI BORA KULIKO VIDONGE
Utumiaji wa vidonge vya Vitamin C hauwezi kutoa faida za kinga sawa kama kunywa glasi moja ya juisi halisi ya machungwa, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kitengo cha Virutubisho vya Binadamu cha Chuo Kiuu cha mjini Milan, Italia. Hii ina maana kwamba ukinywa juisi halisi ya machungwa utapata faida za kinga zaidi kuliko kula vidonge vyake (food supplements).
Kwa kutambua faida za kiafya zinazopatikana kwenye Vitamin C, si jambo la kushangaza kuambiwa na watafiti wetu kwamba ulaji wa matunda na mboga zenye kirutubisho hicho kwa wingi, vina uhusiano mkubwa wa kupungua, kwa kiasi kikubwa, kwa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa moyo, kiharusi na saratani. (Heart Disease, stroke and cancer).
CHUNGWA CHANZO KIZURI CHA 'FIBER'
Faida za kiafya za chungwa zingali zikiendelea hadi kwenye kirutubisho kingine kinachojulikana kama 'fiber' au ufumwele. Tunaelezwa kwamba chungwa moja tu hutoa asilimia 12.5 ya kiwango cha ufumwele kinachotakiwa kwa siku katika mwili wa binadamu, kirutubisho hiki kimeonesha uwezo mkubwa wa kupunguza mafuta mabaya mwilini (cholestro). Vile vile ufumwele unasifika kwa kudhibiti kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni tunda muhimu kwa wangonjwa wa kisukari, hasa wanapokula pamoja na nyama yake.
Kwa kuongezea, sukari ya asili inayopatikana kwenye chungwa (fructose), inaweza kusaidia kudhibiti kupanda kwa kiwango cha sukari mara baada ya mgonjwa kula chakula. Vile vile ufumwele unaopatikana kwenye chungwa una uwezo wa kuondoa viwakilishi vinavyosababisha saratani ya utumbo kwa kutoa utandu wa kinga kwenye tumbo.
Mbali na hilo, machungwa pia hutoa nafuu kwa watu wanaosumbuliwa na tumbo au ugonjwa wa kuharisha. Kula chungwa na nyama yake ili upate faida zote zinazopatikana kwenye virutubisho vilivyomo kwenye tunda hilo.
CHUNGWA HUONDOA MAWE KWENYE FIGO (Kidney stones).
Kama unataka kujikinga na ugonjwa wa kupatwa na mawe kwenye figo, basi unashauriwa kunywa juisi ya machungwa! utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa kwenye jarida la masuala ya lishe la Uingereza (British Journal of Nutrition), uligdundua kwamba wanawake walipokunywa nusu lita mpaka lita moja ya juisi ya machungwa au zabibu kila siku, usafishaji wa njia ya mkojo uliongezeka hivyo kuondoa kabisa hatari ya kuwa na mawe kwenye figo (calcium oxalate stones).
CHUNGWA HUTOA KINGA DHIDI YA VIDONDA VYA TUMBO.
Chungwa moja kwa siku, linaweza kukusaidia kukupa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Chuo cha Lishe cha nchini Marekani ambapo zaidi ya watu wazima 6000 walifanyiwa utafiti kuthibitisha hilo.
HITIMISHO
Kwa ujumla, hizo ni faida chache tu na muhimu zinazopatikana kwenye tunda hili, lakini kuna faida nyingine nyingi tu. Kimsingi tunashauriwa kula matunda ya aina mbalimbali kwa wingi kadri tuwezavyo, kwani kwa kufanya hivyo tutajihakikishia upatikanaji wa faida zote za kiafya zilizomo kwenye matunda.
Kwa kula matunda mengi na mchanganyiko, ndiko kunakoweza kukupa kinga ya mwili na afya njema iliyohuru na maradhi sugu kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kiharusi, kisukari, n.k.
Mungu ametupa matunda mchanganyiko yanayopatikana mwaka mzima katika vipindi tofauti, kwa sababu maalum. Hivyo ni kosa kubwa sana kuacha kutumia matunda haya ya msimu kila yanapopatikana na ni makosa makubwa kiafya kujenga tabia ya kutokula tunda la aina yoyote hata kwa mwaka mzima. Kuanzia leo anza kulithamini chungwa na kuliona kama mkombozi wa afya yako.

EmoticonEmoticon