![]() |
Mkuu wa Wilaya Chunya Mkoani Mbeya Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda hicho |
![]() |
Mtendaji mkuu wa kampuni ya saruji Mbeya (Lafarge)Catherin Langreney akitoa taarifa ya utoaji wa msaada huo |
(Picha na Fahari News)
Jumla ya mifuko 1000 ya saruji sawa na tani 50 yenye thamani ya Sh15milioni imetolewa na Kampuni ya saruji Mbeya (Mbeya cement) kwa serikali Wilayani Chunya kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha michezo Wilayani humo.
Ujenzi wa kiwanja hicho Chunya unatarajia kugharimu kiasi cha fedha Sh 8bilioni ambapo tayari ujenzi wake umeanza wilayani ambapo Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 50,000 pia unatarajiwa kuwa kitega uchumi kwa halmashauri ya wilaya ya Chunya na mkoa wa Mbeya.
Akizungumza wakati wa kukabidhi saruji hiyo Mtendaji Mkuu wa Mbeya Cement Catherine Langreney alisema kuwa kampuni yake imepokea maombi hayo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya na kukubali kuchangia saruji mifuko 1000 baada ya kugundua kuwa uwanja huo utaweza kutoa ajira kwa vijana wengi na kuendeleza michezo.
Langreney alisema kuwa ksmpuni hiyo imekuwa ikichangia huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi waliopo maeneo ya karibu na kiwanda hivyo, msaada huo ni sehemu ya huduma zao za kawaida kwa wananchi.
Aidha alisema kuwa uongozi wa kiwanda hicho unajipanga kutambulisha tekonolojia za kujenga nyumba bora kwa gharama nafuu kwa lengo la kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro alisema kuwa uwanja huo unajengwa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo pendekezo la ujenzi wa uwanja huo aliliwasilisha kwenye vikao vya halmashauri na kuridhiwa na baraza la Madiwani.
Amesema katika vikao vyake, ambapo Halmashauri ya wilaya hiyo ilipendekeza kutenga Sh 70milioni katika bajeti yake ya kila mwaka huku kila mwananchi akiwajibika kuchangia ujenzi wa uwanja huo kuanzia sh.2000 kwa kila mwaka ambapo matazamio uwanja huo unatarajia kukamilika 2016.
Amesema kuwa fursa ya kuwepo kwa uwanja huo wa kisasa itainua michezo ndani ya wilaya hiyo na mkoa wa Mbeya kwa ujumla hivyo wadau wanapaswa kujitokeza kuchangia maendeleo ya uwanja huo.
SOURCE FAHARI NEWS
EmoticonEmoticon