WAPIGANAJI WA BOKO HARAM TAARIFA KUTOKA KASKAZINI MASHARIKI MWA NIGERIA ZINASEMA KUWA ZAIDI YA WANAWAKE 60 WAKIWEMO WASICHANA WA UMRI MDOGO WALIOTEKWA NYARA MWEZI JANA NA BOKO HARAM WAMEKWEPA.TAARIFA HII INAKUJA WAKATI SAWA NA TAARIFA ZA KUTOKEA MAKABILIANO MAKALI KATI YA JESHI LA NIGERIA NA WAPIGANAJI WA KUNDI HILO.
Serikali ya Nigeria imeitisha uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa nyara mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa Kaskazni Mashariki mwa jimbo la Borno.Hali ya usama ni mbaya sana huku miundo mbinu duni ikichangia kuifanya hali ngumu kuweza kufikia maficho ya kundi hilo na pia kubaini idadi ya wasichana waliotoroka kutoka mikononi mwa Boko Haram.
BBC imeongea na jamaa ya wasichana watatu ambao walitoroka. Sasa wako salama nyumbani kwao na mmoja wao amesema kwamba wasichana wengi wamefanikiwa kutoroka.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi.
Maafisa wakuu hata hivyo bado hawajaweza kuthibitisha kukwepa kwa wasichana hao.
Wakati huohuo hapajakuwa na taarifa zozote kuhusu wasichana 200 waliotekwa nyara katika shule ye mabweni ya Chibok mwezi Aprili.
Hatua ambayo imekemewa vikali na jamii ya kimataifa huku baadhi ya mataifa kama vile Marekani, Uingereza na hata Ufaransa wakijitolea kuisaidia serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana hao.
CHANZO: BBC
EmoticonEmoticon