TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.07.2014.






MTU MMOJA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MOMBA.


MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BAKARI DAMSON (27) MKAZI WA MAJENGO AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI ADC 3671 AINA YA TOYOTA LAND CRUISER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA FRANK MATHEW SIKONGA (29) MKAZI WA CHIPAKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.07.2014 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO KATIKA MTAA WA MWAKA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA AMEKAMATWA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.




Imetolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.




Previous
Next Post »