TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 01.07.2014.





·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA MWINGINE KUJERUHIWA BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI.

·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.


·         WATUHUMIWA SABA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA RAHABU KIHANIKU (60) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA  KUFIKISHWA HOSPITALI YA  SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.343 CMQ AINA YA HONDA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA NDULA MWASANGAJA (32) MKAZI WA MTAA WA BAGAMOYO –TUKUYU.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KIKOTA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU.

AIDHA KATIKA AJALI HIYO MTOTO ANGEL OSWARD (02) MKAZI WA KIKOTA ALIYEKUWA AMEBEBWA NA MAREHEMU AMEVUNJIKA MGUU WA KUSHOTO NA AMELAZWA HOSPITALI YA  SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA MAENEO YENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI.
 

KATIKA TUKIO LA PILI:

MTU MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 19-20 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA 22:14 USIKU KATIKA MTAA WA MBILINYI - SAE, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
 


TAARIFA ZA MISAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1. JELY EVARIST (24) MKAZI WA MWANJELWA 2. STAFORD NGENZI (21) MKAZI WA MWANJELWA, 3. ALAN AGUSTINO (23) MKAZI WA ILEMI 4. ASIFIWE ABSOLOM (22) MKAZI WA JUA KALI 5. DATI SAMWEL (24) MKAZI WA MWANJELWA 6. MWAKISYE NAZARETH (23) MKAZI WA MWANJELWA NA 7. MICHAEL EZEKIEL (40) MKAZI WA NZOVWE.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MAENEO TOFAUTI JIJINI MBEYA WAKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 429. MSAKO ULIFANYIKA KATIKA MAENEO YA JUA KALI, MAKUNGULU NA MAJENGO MAPYA, KATA ZA ILEMI NA NZOVWE, TARAFA ZA SISIMBA NA IYUNGA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA  23:30. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA BHANGI.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.



Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »