JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya, Bwana Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa Saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Lbya.
Inataarifiwa kuwa Bwana Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto. Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini. Walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa alikwisha kufariki na Polisi walithibitisha kifo hicho.
Maiti imehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat kwenda Nyumbani kwa mazishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi hiki kigumu.
IMETOLEWA NA
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat kwenda Nyumbani kwa mazishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi hiki kigumu.
IMETOLEWA NA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam
Julai 2,2014
Dar es Salaam
Julai 2,2014
EmoticonEmoticon