Ripoti: Oscar Pistorius yuko kwenye hatari ya kujiua


Ripoti ya wanasaikolojia inaeleza kuwa mwanariadha Oscar Pistorius yuko kwenye hatari ya kujiua kwa kuwa ana matatizo makubwa ya kisaikolojia hivi sasa.
Ripoti ambayo ilisomwa na mwanasheria wa upande wa utetezi inaeleza kuwa Ocar Pistorius alikuwa akiombeleza kifo cha girlfriend wake Reeva Steenkamp aliyemuua kwa kumpiga risasi.
Hata hivyo ripoti ya Jumatatu ya madaktari iliyosomwa mahakamani ilieleza wazi kuwa Oscar Pistorius hakuwa na tatizo lolote la akili usiku aliotekeleza tukio hilo la mauaji.
Mwanariadha huyo mlemavu ameendelea kushikilia utetezi wake kuwa alimpiga risasi mpenzi wake baada ya kudhani kuwa ni mtu aliyevamia katika nyumba yake.
Waendesha mashitaka wanaeleza kuwa uchunguzi unaonesha mwanariadha huyo alimuua mpenzi wake baada ya kuwepo mabishano kati yao.
Marehemu Steenkamp alikuwa mwanamitindo na mhitimu wa shahada ya masomo ya sheria.
Previous
Next Post »