NEYMAR KUIKOSA UJERUMANI NUSU FAINALI, AKIMBIZWA HOSPITALI, SCOLARI ATHIBITISHA

Agony: Neymar lies in agony after being kneed in the back just three mintues from the end
Neymar akiwa amelala chini baada ya kupata majeruhi ya mgongo dakika tatu kabla ya mechi kumalizika. 
NYOTA wa Brazil, Neymar,  ataikosa mechi ya nusu fainali baina ya wenyeji dhidi ya Ujerumani jumanne ijayo, hii ni kwa mujibu wa kocha, Luiz Felipe Scolari.
Taifa mwenyeji limefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Fortaleza, lakini nyota wake alitolewa nje kwa machela dakika tatu kabla ya mechi kumalizika na amekimbizwa hospitali baada ya mechi kumalizika kutokana na kupata majeruhi ya mgongo.
Neymar amekuwa akijikaza kuimarika katika mechi zote za Brazil kutokana na majeruhi ya  goti, lakini alifaulu kuanza katika mechi zote.
Stretchered off: Neymar is carried away by medics leaving all Brazilian fans in a state of panic
Hapa machela: Neymar akitolewa nje ya uwanja kwa machela, huku akiwaacha mashabiki na taifa zima likiwa katika hofu kubwa.
Carried away: Neymar was stretchered off the pitch and taken to hospital after Brazil's quarter-final win
 Neymar alitolewa nje kwa machela na amekimbizwa hospitalini baada ya kumalizika kwa mechi ya robo fainali ya Brazil ambayo wamepata ushindi wa mabao 2-1.
none
Cynical: With the ball nowhere near Juan Zuniga smashes his knee into the lower part of Neymar's back
Juan Zuniga akimgonga Neymar mgongoni kwa goti 
Man down: The Barcelona forward falls to the ground after the challenge that leaves him a doubt for the semi
Mtu chini: Mshambuliaji wa Barcelona  akianguka chini baada ya kugongwa mgongoni na sasa yupo katika wasiwasi mkubwa wa kucheza nusu fainali.
End of the line? Neymar is carried down the tunnel amid fear that his World Cup could be over


STAA wa timu ya Brazil, Neymar hataendelea na michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kuvunjika mfupa unaoshikana na uti wa mgongo wakati wa mechi yao na Colombia usiku wa kuamkia leo.

Neymar akitolewa nje ya uwanja wakati wa Robo Fainali dhidi ya Colombia.
Staa huyo mwenye mabao manne mpaka sasa kwenye michuano hiyo, alitolewa uwanjani dakika tatu kabla ya mechi yao dhidi ya Colombia kumalizika.
Neymar akiwa chini baada ya kuvunjika mfupa.
Katika mechi hiyo, Brazil walishinda mabao 2-1 na kutinga Nusu Fainali ambapo watakutana na Ujerumani Julai 8 mwaka huu.
Hivi ndivyo Neymar alivyoumia.
Kwa mujibu wa taarifa za daktari wa timu ya Brazil, Neymar atakaa nje kwa takribani wiki nne.
Neymar akipatiwa huduma ya kwanza.
Wapenzi wa soka nchini Brazil wakiwa nje ya hospitali aliyopelekwa Neymar.



Ndio mwisho wake? Neymar akiwa amebebwa kwa machela na kuna wasiwasi kuwa inaweza kuwa mwisho wa kucheza kombe la dunia mwaka huu.

Mshambuliaji huyo wa Barcelona amefunga mabao manne katika fainali za mwaka huu, lakini alishindwa kuongeza dhidi ya Colombia kabla ya kutolewa nje kwa machela dakika tatu kabla ya mechi kumalizika.

Kocha wa Brazil Luiz Felipe Soclari alisema: "Sidhani kama ataweza kucheza mechi ijayo".
"Amekimbizwa hospitali binafsi na madaktari kwasababu aligongwa na goti katika mgongo wake".
" Alikuwa analia kwa maumivu. Haitakuwa rahisi kwake kuimarika kwa kuzingatia ukweli kwamba ni majeruhi ya mgongo na maumivu aliyonayo ni makubwa. Acha tuwe na matumaini kuwa kila kitu kinakwenda vizuri".
Previous
Next Post »