Mwili wa Kaimu Balozi wa Libya nchini, Ismail Nwairat (39), umesafirishwa jana kwenda Libya na shirika la ndege ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka Ofisi ya Mawasiliano ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mwili wa balozi huyo anayedaiwa kujiua kwa risasi Jumanne wiki hii mchana akiwa ofisini kwake, mwili wake utapokewa na ndugu zake.
Na kwamba taarifa zaidi juu ya maziko ya balozi huyo zitatolewa na ndugu zake baada ya kuupokea mwili huo nchini Libya.
Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi wa kifo cha kaimu balozi huyo umeanza na kwamba watachunguza sababu za kujiua.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mkumbwa Ally, tukio hilo limeshtua Tanzania kwa kuwa si jambo la kawaida kwa mwanadiplomasia kujiua..
EmoticonEmoticon