Mkazi wa Kijiji cha Nyasoro wilayani Rorya mkoani Mara, Ernest Zabron (60) amehukumiwa kwenda jela miezi sita kwa kosa la kumpiga mkewe Esther Ernest (42) kwa rungu na kumvunja mguu wake wa kushoto.
Hata hivyo, Zabron katika utetezi wake hakuonesha kujutia kumshambulia mkewe na kumvunja mguu.
Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 537/2011 ilisomwa Juni 30 mwaka huu na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Odira Amworo.
Awali mwendesha mashitaka wa Polisi, Abel Kazen alidai mbele ya hakimu kuwa Zabron alimshambulia mkewe katika ugomvi wao uliotokea Saa 2:00 usiku wa Desemba 7 mwaka 2011 nyumbani kwao katika Kijiji cha Nyasoro.
Upande wa mashitaka ulileta mashahidi wawili na PF3 inayoonesha kuvunjika mguu wa kushoto wa Esther kutokana na kipigo.
Ernest, mbali na kukana mashitaka mahakama ilidai kuwa hakuonesha kujutia kitendo alichofanya cha kumshambulia mzazi mwenzake na kumvunja mguu na kumsababishia ulemavu.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Odira alisema, "kutokana na kuonesha ukorofi na kutojutia kitendo ulichomfanyia mzazi mwenzako na kuhukumu kwenda jela miezi sita bila faini ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo".
EmoticonEmoticon