Majeruhi 6 kati ya 35 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga baada ya kupata ajali wakati wakisafiri na gari aina ya fuso,lililopinduka jana asubuhi katika eneo la Uchunga wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga wamepelekwa katika hospitali ya rufaa jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu zaidi.
Majeruhi wengine 11 jana walikimbizwa katika hospitali ya Kolandoto.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Daniel Maguja amewataja waliopelekwa Bugando kuwa ni Masanja Kishiwa 42 mkazi wa Mwajiginya),Mayala Lugomela (31 mkazi wa Jijongo,Malando Mashamindi(20) mkazi wa Nobola,Marco Bundala 19 mkazi wa Jijongo, Jeremia Jisena 35 mkazi wa Mwaweja na Ndila Shigela 41 kutoka kijiji cha Mwajiginya wilayani Kishapu.
Amewataja waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo kuwa ni ni Charles Makengwa, Difa Shimo miaka 28 wote wakazi wa wilaya ya Kishapu na kwamba maiti moja ndugu zake bado hawajapatikana ili kuitambua.

EmoticonEmoticon