Askofu Alinikisa Cheyo anayeshinikizwa kujiuzuru.
Mchungaji Edward Chilale, Mwenyekiti wa Baraza la wazee Usharika wa Bethrehemu na mwenyekiti wa kikao kilichotoa tamko
HALI YAZIDI KUWA TETE NDANI YA KANISA LA MORAVIANI JIMBO LA KUSINIMAGHARIBI, WATAKA ASKOFU AJIUZURU.KANISA LA MORAVIAN TANZANIA,JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI,USHIRIKA WA BETHLEHEMU,S.L.P. 905,MBEYA28/06/2014ASKOFU ALINIKISA CHEYO,JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI,S.L.P 377,MBEYA.YAH: KUJIUZURU NAFASI YA UASKOFU ASKOFU ALINIKISA CHEYOTafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu chahusika.Baraza la Wazee Kanisa la Moravian Ushirika wa Bethlehemu lililofanyika tarehe 28/06/2014katika ajenda zake mojawapo walijadili kuhusu mgogoro unaoendelea katika Jimbo la KusiniMagharibi. Wajumbe walijadili kwa kina kuhusu mgogoro huo na kupitia mambo mengi hivyowaliamua kuwa ili kulinusuru Kanisa kuendelea kuwa na migogoro isiyo ya lazima linatoatamko kuwa Askofu Alinikisa Cheyo ajiuzuru mora moja ili kuleta amani ndani ya Jimbo letu.Mchanganuo kuhusu mgogoro huo umeambatanishwa.Tunakutakia utelekezaji mwema,
………………………………………………
…………………………………………
MWANDISHI M/KITI WA BARAZA LA WAZEEUSHIRIKA USHIRIKA WA BETHLEHEMU NakalaMkuu wa WilayaMkuu wa Wilaya wa polisi (OCD)Wakuu wa Idara na Taasisi za KanisaShirika zote za JimboTAARIFA YA UCHAMBUZI WA MGOGORO WA HALMASHAURI KUU YA JIMBO,JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI (JKM) DHIDI YA MWENYEKITI MCH. NOSIGWEBUYA NA UHUSIKA WA ASKOFU ALINIKISA CHEYO Ndugu zangu wapendwa, mgogoro huu umeleta madhara makubwa katika Kanisa, na kuligawaKanisa letu katika vipande vipande ambalo katika historia yake. Mgogoro huu umesababishakutoelewana kati ya uongozi wa Jimbo wao kwa wao, Halmashauri kuu ya Jimbo, kamati tendajina kuleta migongano kati ya Kamati tendaji na Shirika, wachungaji kujigawa katika makundi.Hivyo mgogoro huu umeleta uhasama kati ya mchungaji na mchungaji, ushirika na ushirika,mchungaji na wakristo wake, uhasama usiokoma. Wachungaji kutoelewana na uongozi waWilaya, Mtaa n.k. Hili jambo ni kubwa ingawa wengine wanatofautiana kimtazamo, viongozi wa juu wa Kanisa, Wachungaji na Wakristo kwa ujumla. Lakini ukweli kuwa jambo hili ni kubwana lina madhara makubwa kwa Kanisa na endapo halitapatiwa ufumbuzi litazidi kuleta madharamakubwa zaidi. Uchambuzi wetu kuhusu jambo hili tumeona kuwa linamhusu sana AskofuAlinikisa Cheyo kuwa mhusika mkuu wa chanzo cha tatizo la mgogoro huu kwa kukiuka Katibaya Kanisa letu mara kadha, kiasi kwamba amebadilisha nafasi yake ya Uaskofu na kuwamtendaji mkuu badala ya kulisimamia Kanisa kwa ushauri na usuluhishi. Yeye ameingiakiutendaji zaidi na dhamiri ya kumuondoa Mwenyekiti Mch. N. Buya huku akijua kabisa kuwaanafanya makosa ya kikatiba kwa kufanya mapinduzi, rejea Katiba ya KANISA LA
MORAVIAN TANZANIA JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI IBARA YA 33, KUFUNGU B,
Kipengele cha namba tatu ya kirumi (III) wajibu wa Askofu “………….wote wanaweza
kumwendea kwa shida zao za kiroho moja kwa moja, yeye huwashauri, huwaonya, huwafariji nakuwaongoza kiroho bila kukata mambo yeyote kisheria na kuyapeleka kwenye Halmashauri kuu
ya Jimbo”
Pia alichukuwa nafasi ya maamuzi ambayo yeye kikatiba siyo Mwenyekiti, hapa pia alikiukaKatiba, Ibara ya 33, Kifungu B, kipengele cha namba nane ya kirumi (viii)
“Rejea Katiba“………….Anaweza kukaribishwa katika vikao vya kamati tendaji.”
Hivyo uchambuzi upo kama ifuatavyo:-Mwanzo wa chimbuko la mgogoro ilitokea mnamo tarehe 30/04/2013 ambapo Halmashauri kuu jimbo ilikutana Agenda ilikuwa kujadili utendaji mbovu wa kamati tendaji. Na katika kikaohicho walimtaka Mwenyekiti atoe taarifa ya Tshs 200,000,000/= (millioni mia mbili) zaSekondari za ujenzi wa shule. Na vilevile Makamu Mwenyekiti Z. Sichome alikuwa ameagizwaalete taarifa ya maandishi ya jinsi anavyotimiza wajibu wake kikatiba, kusimamia majengo,kufuatilia mkopo wa ujenzi wa Tshs Millioni mia mbili (200,000,000/=) , taarifa yakeikakataliwa maana haikuonyesha jinsi alivyotimiza wajibu wake, rejea IBARA 35, KIFUNGU
CHA 2 wajibu wa Makamu Mwenyekiti kipengele F. “ Kuangalia kazi zote za majengo katika
Jimbo akishirikiana na Mwenyekiti wa Wilaya ambapo majengo yapo na kutoa taarifa kwa
Kamati tendaji kwa utekelezaji”. Kikao kiliona kina uwezo wa kuamua maamuzi magumu bila
kuvunja amani, hivyo Askofu aliamrisha Kamati tendaji watoke nje ya kikao (Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na katibu) kisha kikao kilikwenda mbali zaidi kikamtoa mtunza hazina namkaguzi wa ndani nje ya kikao. Hivyo safu yote ya uongozi huo ikawa nje ya kikao. Baada yahapo akachaguliwa Ndugu Hakimu Mwandenuka kuwa Mwenyekiti wa kikao cha Halmashaurikuu ya Jimbo kwa uamuzi huo ulikiuka Katiba Ibara 10: 2
C rejea “Kamati tendaji”
Mwenyekiti
na Makamu wawe wachungaji”
Imekuwaje Mkristo asiye Mchungaji achaguliwe
|
EmoticonEmoticon