EEE MUNGU TUSAIDIE ONYO PICHA ZINATISHA: MIILI ZAIDI YA 50 YAKAMATWA BUNJU, DSM IKIENDA KUTUPWA

Viungo hivyo vilikuwa vibichi na baadhi vikivuja damu vilikuwa vinapelekwa kutupwa kwenye dampo la Mpiji. Imedaiwa kuwa gari hilo lilifanikiwa kufanya safari ya kwanza ambapo liliweza kumwaga viungo kama hivyo katika eneo hilo la Mpiji, karibu na shule ya Consolata, shule inayomilikiwa na kuendeshwa na Masista wa kanisa Katoliki.
Imedaiwa alipokuwa anakwenda mara ya pili ndipo wananchi walioshuku tukio hilo waliwashtua polisi na kisha kufanikiwa kumkama ta dereva wa gari hilo.
Umati mkubwa wa wananchi wenye hasira kali ulizingira eneo hilo kwa nia ya kutaka kumuua dereva huyo, iliwalazimu polisi kupiga risasi hewani ili kutawanya umati huo katika eneo la Bunju A.

Immamatukio ilimtafuta Kamanda wa Mkoa wa Kindondoni kupata maelezo zaidi lakini hatukufanikiwa, tutaendelea kuwapat taarifa leo, fuatilia hapa


Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari usiku huu ni kuwa gari dogo lenye usajili T166CAF aina ya Isusu imekamatwa na polisi likiwa na viungo vya binadamu vilivyokuwa vimefungwa katika mifuko ya plastiki.

Walioshuhudia tukio hilo wamedai kuwa gari hilo lenye uwazi mfano wa kenta iliyowazi ilikuwa imejaza viungo mbalimbali vya binadamu vikiwa mimefungwa katika mifuko myeusi ya plastiki ikiwa ni pamoja na vichwa, miguu, mikono na vingingevyo.
.

ANGALIA PICHA ZAIDI WARNING: ZINATISHA




Previous
Next Post »