DJ Khaled ameamua kurusha karata yake kwenye biashara ya headphones, biashara iliyomgeuza Dr Dre kuwa billionaire.
DJ huyo wa Miami alitangaza kupitia Instagram kuwa amejiunga na Heads Audio na Bang Olufsen kuhakikisha anatengeneza headphones bora zaidi katika soko la muziki alizozipa jina la ‘We The Best Sound’.
“Today I am proud to announce that I have partnered with Heads Audio & Bang Olufsen to create the best audio in the market place, We The Best Sound.” Ameandika DJ Khaled kwenye tangazo lake refu linaloahidi makubwa.
Wasanii wengine ambao wana biashara ya headphone ni pamoja na 50 Cent, Ludacris na Dr.Dre.
Biashara hiyo ilimfanya Dr Dre kuwa billionaire baada ya kampuni ya Apple kuamua kununua kampuni ya Beats Electronics mwezi uliopita.
Tayari wasanii wengi wameanza kumuunga mkono DJ Khaled katika biashara hiyo akiwemo Fat Joe, Flo Rida na French Montana ambao amepost picha zao wakiwa wamevaa headphones za We The Best Sound.
EmoticonEmoticon