Daraja laua na kujeruhi katika mji yanapofanyika mashindano ya Kombe la Dunia


Watu wawili wanaripotiwa kufa na 22 wamejeruhiwa baada ya daraja linalopita juu ya barabara kuvunjika katika mji wa Belo Horizonte ambako baadhi ya mechi za kombe la dunia zinafanyika.
Daraja hilo limeripotiwa kuvunjika Alhamisi ya iliyopita na kuvunja sehemu ya basi huku gari lingine likiwa limenaswa ndani.
Wajenzi wa daraja hilo walipaswa kuwa wamemaliza ujenzi kabla mashindano ya Kombe la Dunia kuanza.
Mji wa Belo Horizonte umesha-host mechi 5 za kombe la dunia hadi sasa na ndipo mocha nyingine ya nusu fainali itafanyika.
Previous
Next Post »