Video: Bomu lalipuka na kuua 21 katika duka kubwa la manunuzi Abuja, Nigeria

Shambulizi baya la bomu limesababisha vifo vya watu 21 na kujeruhi mamia katika duka kubwa la manunuzi ‘Mall’ jijini Abuja, Nigeria.
AFP imeripoti kuwa bomu hilo limeripuka katika duka la manunuzi la Emab Plaza lililo karibu na Banex Plaza, maduka ambayo huwa na wateja wengi kuliko maduka yote (mall) katika jiji hilo.
“Unaona moshi mkubwa unafuka angani. Ni sehemu ya watu wengi.” Msemaji wa kitengo cha dharura cha Abuja aliiambia AFP.
Ripota wa Vanguard aliyekuwa kwenye eneo la tukio alisikika akiripoti kuwa anaona vipande vya miili ya watu katika eneo hilo na kwamba bado kuna watu wafanyabiashara wengi na watu waliotembelea Mall hiyo wamenasa kwenye jumba hilo.
Zaidi ya ambulance 6 zilionekana zikitoka kwenye eneo la tukio likiwa limejaza majeruhi.
                                                   

Previous
Next Post »