TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 24.06.2014.




·         MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MOMBA.


·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA TOFAUTI.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 23.06.2014 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU KATIKA ENEO LA CHAPWA, KATA YA CHIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. MAREHEMU ALIKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.419 BRA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. JITIHADA ZA KULITAFUTA GARI NA DEREVA ZINAFANYWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

TAARIFA ZA MISAKO:

MSAKO WA KWANZA:

MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JULIUS ERNEST (27) MKAZI WA KANGA, WILAYANI CHUNYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIUZA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA  BOSS PAKETI 15.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 23.06.2014 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KANGA MADUKANI, KATA YA   KANGA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA AMEFIKISHWA MAHAKAMANI CC 98/2014 NA KULIPA FAINI TSHS 100,000/= -ERV 50360638.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII NA WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

MSAKO WA PILI:

MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BWIGANE MKAMBALA (32) RAIA NA MKAZI WA NCHINI MALAWI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA AMEINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 23.06.2014 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI KATIKA MAENEO YA BULYAGA, KATA YA BULYAGA, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MHAMIAJI HARAMU, TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UPELELEZI DHIDI YAO UFANYWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »