TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 13.06.2014.



·         WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NOTI BANDIA.

·         MFANYABIASHARA MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.


TAARIFA ZA MISAKO:

WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA TATU MWAMPASHI (25) MKAZI WA MPEMBA NA 2. ANGOMWILE KAPUNGU (26) MKAZI WA MTAA WA UNYAMWANGA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NOTI BANDIA.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MAENEO TOFAUTI WILAYANI MOMBA MAJIRA YA SAA 10:30 NA MWINGINE SAA 10:40 ASUBUHI.

MTUHUMIWA WA KWANZA TATU MWAMPASHI (25) ALIKAMATWA KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA, KATA YA KIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA AKIWA NA NOTI BANDIA 31 KILA MOJA IKIWA NA THAMANI YA TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS 155,000/=ZOTE ZIKIWA NA NAMBA AA0845926.

AIDHA MTUHUMIWA WA PILI ANGOMWILE KAPUNGU (26) ALIKAMATWA KATIKA KITONGOJI CHA SIKANYIKA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA AKIWA NA DOLA BANDIA 2 @ THAMANI YA   USD 100 ZIKIWA NA NAMBA BL-72830434-A NA FT-85311229-H.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYWA.

KATIKA MSAKO MWINGINE:

MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAILOS KAYANGE (45) MKAZI WA MBOZI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA VIPODOZI MBALIMBALI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 12.06.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI KATIKA MTAA WA MWAKA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. VIPODOZI HIVYO NI PAMOJA NA BELTASON DAZANI 10, EPIDERM DAZANI 4 NA CARLORIGHT KATONI 01 ZOTE ZIKIWA ZIMETOKA NCHINI ZAMBIA.  

TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII/WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UINGIZAJI NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA MTANDAO WA UTENGENEZAJI NOTI BANDIA HAMA UINGIZAJI NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »